
Pichani ni kiumbe wa majini kwa jina la kitaalamu ajulikana kama isopod. Basi huyo makazi yake ni ndani ya mdomo wa samaki na kazi yake ni kuula ulimi wa samaki hadi akaumaliza wote na kisha yeye kuchukua nafasi ya ulimi huo na kuwa kama ulimi mpya wa samaki. Waliomsoma mdudu huyo wanasema hasababishi maumivu yoyote kwa samaki (sasa mi hata sijui walichunguza vipi wanasayansi hao hadi wamejua kama kweli hasababishi maumivu?) mwe, na teknolojia hii, huenda ishagundulika namna ya kuwasiliana na samaki akatolea maelezo ikiwa anapata maumivu ama la.
Wataalamu hao wanadai kuwa kidudu hiki hakina madhara yoyote katika mwili wa binadamu isipokuwa tu pale utakapotaka kukakamata kakiwa hai, basi katakudunga kwa vijisindano uchungu vyake.
Nimemtizama mdudu huyo nikasikia mwili wanisisimka na vipele vya kuku vyanitoka ghafla!
Mvuvi mmoja aliyewahi kukumbana na kidudu hichi anasema: "Really quite large, really quite hideous - if you turn it over its got dozens of these really sharp, nasty claws underneath and I thought 'that's a bit of a nasty beast'." And while it can't seriously hurt people, it evidently doesn't like them: "It doesn't affect humans other than if you do actually come across a live one and try and pick it up - they are quite vicious, they will deliver a good nip."





RSS Feed