Tetemeko la ardhi lililotokea Februari 27 muda wa ya saa tisa usiku wa manane (majira ya Chile) katika eneo la Pasifiki limesababisha athari kubwa nchini Chile ikiwamo vifo vya watu wapatao 200. Tetemeko hilo limesababisha Tsunami katika bahari ya Pasifiki na maeneo yanayoizunguka. Mashirika ya uokozi pamoja na usalama yanajiweka katika hali ya utayari ili kupambana na athari za mabadiliko ndani ya bahari itakayoleta athari katika eneo la nchi kavu.
Mwenyezi Mungu azilaze pema roho za marehemu hao. Amin.