Bodi ya Mikopo vs Wahitimu Vyuo Vikuu 03/02/2010
Kwa heshima zote naomba bwana Ojung Longdare apokee ombi langu la kuweka habari hii aliyofahamisha watu wengine wa kundi pepe fulani, nami nikaona vyema kila mhitimu anayedaiwa na Bodi ya Mikopo asome ujumbe huu na ajue hatua ya kufuata. Kuna taarifa nilizopokea muda mfupi uliopita na ningependa niwashirikishe. Kwa muda sasa Higher Education Students Loarn Board imekuwa ikipanga mkakati wa kufuatilia wadaiwa hasa waliohitimu vyuo vikuu kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka jana. Mkakati mmojawapo ni kuwazuia wanaodaiwa pale wanapopita katika viwanja vya ndege wanapoondoka nchini au kuingia kutoka nje. Wadaiwa watashikiliwa viwanjani na kutakiwa kueleza namna watakavyolipa deni. Ili kuepuka usumbufu, inashauriwa kwenda ofisi za HESLB na kujua kiasi cha deni unalodaiwa na kueleza namna utakavyokuwa ukilipa. Utapewa barua itakayokusaidia ikiwa utazuiwa na mawakala watakaokuwepo nchi nzima kufuatilia madeni ya bodi hiyo. Naelewa kwamba suala hili haliwahusu wafanyakazi wa serikali kwa vile wao hukatwa moja kwa moja kutoka katika mishahara yao ya kila mwezi. Pia nakumbuka magazeti hasa Daily News la wiki tatu zilizopita lilitoa majina ya wadaiwa wote Habari hii nimepewa na ndugu yangu aliepita JKNIA jana. Mwenye taarifa zaidi atupatie... Ninapenda kumwomba pia Mwalimu Mathew Mndeme apokee ombi langu la kushiriki maoni yake na Watanzania wengine wapate mwanga kuhusu suala hili. Deni lenyewe ni dogo sana hasa kwa wale ambao walisoma kabla bodi hii haijaanziswa. Wale waliosoma kabla ya kuanzishwa kwa bodi hii mwaka 2004 nadhani wanacholipa ni ile pesa ya kujikimu uliyokua unapewa na ya kwenda field. Ada ilikua inalipwa kama mchango serikali kwa suala zima la cost sharing.....wale waliosoma kuanzia 2004 ndio wanalipa full package ikiwa ni pamoja na ada na mahitaji maalum ya vitengo kama yalikuwepo... Mimi nilipoanzwa kukwata nilikuta deni langu ni kiasi kidogo sana kwani halikuzidi 2M na wananikata kwa kiwango kitakacholipa hili deni kwa miaka kumi hivyo unaweza kuona kulipa ni kazi rahisi sana. Kwa wale wenye uwezo nawatia moyo wakalipe tu vijisenti vyote wanavyodaiwa kwa mkupuo ili tuwaruhusu wadogo na watoto zetu nao kukopeshwa wengi zaidi wakasome. Hasa wale ambo hatujaajiriwa kama wafanya biashara na wanaoendesha miradi yao binafsi...tusione ni ushuhuda kuwa sisi hatukatwi deni....twendeni tukakubaliane na mdai wetu namna bora ya kulipa. Ni aibu mpendwa ukianza kusukumana na akina majembe auction mart kulazimishwa kulipa deni la elimu uliyopitapa. Kwa wasiojua kiasi cha deni wanachodaiwa, inigia kwenye website ya HESLB upate mawasiliano nao ili wakujulishe kiasi cha deni lako na uanze kulipa. Kuna waajiri hawatoi taarifa kuwa wana mtu wamemwajiri na anadaiwa na board kama sheria inavyowataka. Kama unaona hadi leo salary slip yako haioneshi kukatwa deni hili (ikimaanisha mwajiri wako hajareport) ni bora wewe mwenyewe ukachukua hatua ya kiungwana ukawasiliana na board na kuwaambia unapofanya kazi ili uanze kutimiza ahadi yako uliyoitoa kwa maandishi. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed