wavuti
wavuti logo Facebook icon Facebook icon Twitter icon Subscribe RSS
 
...kwa kiasi kikubwa kingeweza kuepukika kulingana na tatizo la afya lililomkuta marehemu. Nasema hivi kwa uzoefu kwa vitendo wachilia mbali nadharia katika masuala ya afya. Ni akina mama wengi na watoto ambao afya zao zimeweza kuboreshwa kwa matibabu mahsusi, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kuahirisha mauti. Matibabu bora hutegemea sana uwepo wa vifaa hitajika na wataalamu wa kutosha, jambo ambalo nchi yetu bado ipo nyuma sana sana. Naisubiri kwa hamu siku ambayo wenye mamlaka wataweka kipaumbele katika masuala muhimu kabisa Afya, Elimu na Miundombinu kwa wananchi kwa maendeleo chanya ya binadamu.
Picture
marehemu Habiba Mkwawa
Kifo cha Habiba Kawawa
Marehemu Habiba Kawawa amezikwa jana jioni huko Moshi katika maziko ambayo mwanasheria wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,NHIF, Christina alipata shida ya kumalizia wasifu wa Marehemu. Habiba aliyezaliwa Desemba 21,1975 jijini Dar es Salaam na kupata elimu yake ya msingi mwaka 1982 hadi 1988 katika shule za msingi za Karume na Kiluvya zote za Dar es Salaam alisomea Sekondri za Weruweru na Kibosho mkoani Kilimanjaro ni mtaalamu wa sheria.

Habiba alipata elimu yake ya sheria IDM - Mzumbe kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 1997 alipofanikiwa kupata diploma ya Sheria.Alijiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam 1998 na kutunukiwa shahada ya sheria mwaka 2001. Juni 15,2006 alifaulu mtihani wa uawakili na kutunukiwa cheti cha uwakili. Wakati anakufa alikuwa anaandika 'thesis' ya digrii yake ya pili ambayo alikuwa akiipata kutoka Chuo Kikuu cha Capetown. Habiba ambaye alikuwa mwanachama wa chama cha Sheria na kile cha wansheria wanawake alishawahi kuwa mwandishi wa habari kwa muda mfupi katika miaka ya 1995 na 1996 katika magazeti ya Habari Corporation chini ya usimamizi wa Jenerali Ulimwengu na John Bwire.

Mwaka 1997 aliingia Halmashauri ya Jiji la dar es salaam kama Afisa wa Sheria Msaidizi na kupanda ngazi kufikia Afisa Sheria mwaka 2001. Mwaka 2006 alijiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya kama Afisa Sheria Daraja la Pili, akapanda cheo kuwa Kaimu Meneja wa Kitengo cha Sheria na mwaka huu aliteuliwa kuwa Meneja Mradi wa Huduma za kinamama wajawazito wasio na uwezo na wanaoishi na virusi vya ukimwi, nafasi aliyoshika hadi umauti unamkuta.

Akiwa kama mtaalamu wa sheria na wakili, Habiba aliwasaidia watu wasio na uwezo wa kifedha mahakamani na kuwatetea. Marehemu Habiba ambaye alikuwa mjamzito usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu ya tarehe Mosi mwezi huu wa Februari alifika hospitalini kuona daktari wake na alimshauri kupumzika hospitalini hapo kuangaliwa mwenendo wa presha yake.

Alhamisi ya tarehe 4 marehemu aliwapa matumaini watu wote waliokwenda kumjulia hali na kuonge anao na hata kusaini baadhi ya nyaraka za ofisi yake ili kuwezesha mchakato wa mradi wa huduma za kminana wajawazito wasio na uwezo na wanaoishi na virusi vya ukimwi uweze kuendelea. Saa kumi jioni hali ilibadilika na saa 11.30 jioni Habiba alifariki dunia. Habiba alifunga ndoa na Johnson Maleko Aprili 29,2000 na katika ndoa yao walibahatika kuwa na mtoto Anna Asia Maleko ambaye sasa ana miaka 7.

Wasifu na habari ya msiba huu ni kwa mujibu wa blogu ya Lukwangule (Beda Msimbe).

Tunaungana na wote waliotoa pole kwa wafiwa na wale walioguswa na msiba huu.
Apate pumziko jema Habiba Kawawa.

 


Comments


Comments are closed.