Hakuna uchaguzi mwaka huu 08/02/2010
Hayo yamesemwa na shehe, mtabiri na mnajimu Yahya Hussein alipokuwa akizungimza kupitia runigna ya Channel TEN katika kipindi cha masaula ya Nyota. Shehe huyu alitoa kauli mwaka jana iliyozua gumzo pale aliposema kuwa "mwanachama yeyote ndani ya CCM atakayesimama kumpinga Rais Jakaya Kikwete katika kinyang'anyiro cha kupata nafasi ya kugombea urais atakufa ghafla", unaweza kubofya hapa kusoma zaidi. Katika utabiri wake wa sasa, Shehe huyo alisema, "nasema hakuna uchaguzi mwaka huu, uchaguzi utaahirishwa, siwezi kusema sana, maana karibuni nilitoa utabiri kuwa kuna mtu anaweza kufa katika kugombea urais, watu wamesema sana". YATOKANAYO Ninachojiuliza ni kwa nini masuala kama haya yanazungumzwa kwenye vyombo vya habari vinavyoifikia jamii kubwa na wahusika hawatoi tamko lolote. Ni kwa kuwa nafasi ya shehe huyu ni kubwa katika jamii ukilinganisha na watu wengine, hivyo angetokea mtu yeyote asiye na madaraka ya kijamii, tungepuuzia, lakini mtuu mwenye ushawishi katika kundi la watu akizungumza, linapewa uzito fulani. Ndiyo maana wanapozungumza wakuu wa dini na madheheu fulani fulani na kutoa tamko, wahusika huchunguza na kukabilianana matamko hayo. Je! wahusika hawaoni kuwa hii la Shehe ni kuingilia msemaji wa Serikali na kutumia vibaya ushawishi alionao katika jamii na kuweza kuzua mtafaruku ama/au chuki miongoni mwa wanajamii? Mi kwa mtizamo wangu nadhani si sawa kusikia kauli zinazohusu suala nyeti la nchi kutoka kwa asiye msemaji wa Serikali, labda iwe aliyesema hivi ndiye ila hatujapewa taarifa rasmi. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed