![]() Hasheem Thabeet Habari zilizoandikwa hivi karibuni mtandaoni kumhusu Mtanzania mwenzetu, kijana Hasheem Thabiti ambaye ni Mtanzania wa kwanza kucheza mchezo wa kulipwa wa mpira wa mikono katika ligi ya nchini Marekani maafuru kama NBA, si za kufurahisha. Hasheem alinyakuliwa katika naasi ya pili 'Pick Number 2' na timu ya Memphis Grizzlies kwa ajili ya msimu wa NBA 2010. Habari zilizoripotiwa na kuandikwa katika mtandao wa Yahoo! na mitandao mingine zinasema kuwa Hasheem ameshushwa kutoka NBA na kupelekwa katika ligi ya D (Developmental League) ambapo mchezaji anayeshindwa kufikia viwango na malengo katika NBA hutakiwa kwenda kwa muda ili kujinoa zaidi. Kitakwimu, katika michezo yote 50 aliyocheza Thabeet msimu huu, ameweza kupata wastani wa pointi 2.5 tu ndani ya kila dakika dakika 10.3 za mchezo. Tayari amepoteza nafasi yake katika timu ya Grizzlies kwa Hamed Haddadi, kiungo wa kati aliyeichezea timu hiyo kwa miaka miwili sasa. Wakala wake, Bill Duffy, alifanya juhudi za kumhamishia kwenye timu ya Dakota Wizards ambayo ni washirika wa Grizzlies katika D-Legue na kusema, "I think he needs to play". Kwa kucheza D-League, Hasheem anakuwa mchezaji wa kwanza kabisa kushuka toka NBA hadi D-Legue kati ya wote waliowahi kunyakuliwa katika nafasi za juu za NBA draft. Hasheem anatarajiwa kuingia kiwanjani wakati Dakota itakapopambana na Erie siku ya Ijumaa. YATOKANAYO Waswahili tuna usemi wetu kuwa, 'kuteleza si kuanguka'. Kwamba kijana Hasheem bado anayo nafasi ya kufanya vizuri na kuwa mchezaji bora kabisa ikiwa atapata ushauri na maelekezo mazuri. Safari ya Hasheem alikotoka na alikofikia si ya lele mama hasa pale utakapoilinganisha na mamilioni ya watu, si tu wanaotoka nje ya Marekani, bali hata waliopo nchini Marekani kwenyewe. Historia ya Hasheem ya nyumbani Tanzania ambako mchezo wa mpira wa kikapu si nzuri kama ilivyo mchezo wa soka, anayo kila sababu ya kuangalia hatua na mafanikio aliyoyafikia. Kwa kuzingatia umri wake (16 Februari 1987), Hasheem bado anayo fursa ya kujinoa, kukata tamaa ni mwiko. Mara zote tunapoanguka au kupatwa na shida, yatupasa kuangalia chanzo cha tatizo, kisha tutafute mbinu sahihi za kulitatua na tena liwe somo ili tupate kujifunza kutokulirudia tena kosa. Binafsi nimejitahadharisha, 'usifurahie kujikwaa kwa mwenzio' ama 'usicheke ukunga na uzazi ungalipo'. Nimepitia magumu mengi, matatizo makubwa, na machungu tele, na bado mapambano yanaendelea, hivyo ninaelewa ilivyo mtu unapopatwa na hisia za uchungu na pengine aibu. Lakini huu si wakati wa kufikiria hayo, huu ni wakati wa kujua kuwa kadiri ya ukubwa wa jina lako, ndivyo utakavyokuwa ukubwa wa mlio wa mguno wako. Kijana jipe moyo mkuu, nyanyuka, simama imara, piga kifua mbele, safari na iendelee. Nasemaje, 'make it your STEPPING stone and not a STOPPING stone' - Subi, 25.02.2010. CommentsDr.Mallaba 26/02/2010 5:03am
I absolutely agree wth Subi on what u have said and I do remember Thomas Edson's quote once he said "
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed