Kuna mjadala mzito unaoendelea huko nyumbani kwenye vijiwe na mablogu kuhusu huyu jamaa aliyeandika hicho kijitabu kinachowabomoa mafisadi wa elimu. Lakini swali ninalojiuliza je huyu jamaa anapowasema hawa ni mafisadi wa elimu aliegemea kwenye kigezo gani hasa (maana bahati mbaya sijafanikiwa kupata nakala ya hako kakitabu nikamsoma). Je ni kwa sababu wana vyeti feki au kwa sababu wamesoma vyuo visivyotambulika duniani (non-accredited colleges and Universities) au kwa sababu wamesoma substandard elimu? Kama ni kufoji vyeti sawa hili ni jambo lililo wazi na linaeleweka na wala halihitaji mjadala kabisa lakini kama ni kutotambulika kwa chuo nadhani hili suala ni pana na linahitaji uchambuzi wa kina. Hivi leo Tanzania tuna baadhi ya vyuo ambavyo ni non-accredited kwa viwango vya TCU na NACTE lakini bado tuna watu wengi waliosoma na wanaoendelea kusoma hapo na kila mwaka registration ya wanafunzi wapya inafanywa lakini sijasikia hizi bodi zikipiga kelele. Nakumbuka miaka fulani huko nyuma kulikuwa na ile issue ya IMTU TCU waliwakomalia mpaka jamaa wakarekebisha mambo fulani walau leo wanatambulika lakini vipi kuhusu chuo fulani hapo Dar ambacho inasemekana hakipo accredited mbona hawapigi kelele zozote. Hii ina maana kama tutabase katika kigezo cha kusoma katika non-accredited vyuos basi mafisadi wa elimu Tanzania watakuwa wengi sana. Kuna suala la kuwa na standards katika elimu. Unaposema standards hapa inabidi tujiulize je tunazungumzia standards za wapi? Tanzania, Japan, Britain, Korea au USA? Maana kila nchi ina standards zake zinazotofautiana ama kidogo au sana na nyingine. Utakuta kozi fulani, kwa mfano, Tanzania inasomwa miaka miwili lakini Australia kozi hiyohiyo mtu ataisoma kwa mwaka mmoja, je huyu akirudi Tanzania utamwambia ni fisadi wa elimu au elimu yake ni substandard kwa vile amesoma kwa mwaka mmoja? Na je yule aliyeisoma kozi hiyo hiyo UK kwa miezi tisa utamuitaje? Kuna baadhi ya nchi kwa mfano hapa China, unaweza kuanza kusoma Masters ya miaka mitatu na ikitokea kwa mfano katika mwaka wa kwanza (unakuwa umesoma basics subjects) ukafaulu vizuri sana unaruhusiwa kuunganisha PhD ambayo utatakiwa kuifanya kwa miaka mitano, kwa maana ya mitatu ya Masters yako na miwili ya PhD na hivi unapograduate mwishoni mwa hiyo miaka yako mitano unapewa vyote viwili, masters na PhD (kwa maana ya MMed/ PhD). Sasa je mtu wa namna hii tutasema ana substandard education kwa vile tu system ya elimu aliyosomea ni tofauti na ya kwetu? Hebu chukulia mtu aliyesomea udaktari Germany, system yao ni tofauti kabisa na Tanzania. Wakati sisi kwetu mtu anasomea MMed kwa miaka mitatu au minne, Germany wao hawana hiyo system ya MMed. So huyu aliyesomea Germany utasema ni substandard kwa vile tu haendani na standards za Tanzania? Kuna mifano mingi mingi ya jinsi standards na systems za elimu zinavyotofautinan kati ya nchi na nchi. Lakini pia suala la standards linaweza kupimwa na mtaala na njia inayotumika katika kufundishia. Sitegemei hata siku moja mwanafunzi wa MD asomee kozi yake online kwa maana katika mtaala wake unamtaka awe darasani kwa masaa kadhaa kwa semester na sehemu nyingine awe wodini ama thietre akishughulika na wagonjwa na kujifunza baadhi ya procedures. Hivyo mtu atakayesema yeye ni daktari aliyesomea kozi yake online huyo moja kwa moja atakuwa feki kwa maana ya elimu yake kuwa substandard. Lakini kuna baadhi ya kozi ambazo nadhani mtu bado anaweza kusomea online na bado akatoka akiwa amewiva kabisa. Kozi kama DS, International Relations, MBA, MPH, MSc. Epidemiology na nyinginezo naamini bado mtu anaweza akazisomea kwa njia ya distance learning na akawiva kabisa. Lakini pamoja na hayo maswali ya kujiuliza hapa ni je hivi vyuo vinatambulika katika kutoa elimu ya njia hii? Je kuna kipindi mwanafunzi anatakiwa kuwa na contact na mwalimu wake? Je muda wa kozi ni sufficient enough kuwezesha topics zote kuwa covered? Je mwanafunzi anapimwaje kuweza kujua kuwa amewiva na anastahili kupewa cheti? Na hapa ndipo issue ilipo. Utakuta chuo kinajitangaza kuwa kinatoa online PhD ya kitu fulani. Ukiuliza muda wa hiyo PhD ni miezi 9!!! Jamani PhD ya miezi tisa kweli?? Hapa ndipo nilipo na tatizo. Ingawa PhD haikuhitaji sana kuwepo darasani lakini bado kule kuandika thesis na kuifanyia kazi ni shughuli tosha ya kukufanya uwe bize kiasi kwamba siamini hata siku moja kama kweli unaweza kuifanya PhD online tena kwa miezi tisa au hata mwaka kama baadhi ya wanasiasa wetu walivyotudanganya na kujipachika mavyeti ya uongo. Lakini je kuna muda uli standard wa kuifanya PhD duniani? Sidhani. Ninavyojua kila nchi ina muda wake minimum ambao walau mtu anatakiwa awe ameutumia kufanya PhD. Kwa mfano nikichukulia China the minimum time ni three years (hii ni nje ya ile system niliyoisema hapo awali). Na hii inatofautiana kati ya nchi na nchi. Poland kwa mfano minimum ni three years lakini kama unaunganisha (wenyewe wanaita fast track PhD kama hiyo ya China) inakuchukua only two years. Sasa leo ukiniambia mtu amefanya PhD online tena kwa miezi tisa hapo kwakweli nitashangaa na kuanza kudoubt. Kwahivi simtetei yeyote aliyesemwa kwenye hicho kijitabu kwa sababu wengi wao sizijui elimu zao lakini najaribu tu kuthink na kuview rationally. Nimeraise hii issue ili siku moja na sisi tusijeambiwa kuwa na elimu za kudesa kwa vile tu tulisomaga fasttrack PhD, MPH au International Health za online. Monsignor, China. CommentsMallaba 13/02/2010 2:23am
Tatizo lililopo hapa kwa hawa watajwa(mawaziri,wakuu wa mikoa na wabunge) ni kuforge wala si kitu kingine.Inaonesha hawa jamaa hawakusoma hata miezi sita online bali walichofanya ni kuforge vyeti kwa makusudi kabisa na hawa watu hawana ujuzi wowote hata kidogo kulingana na vyeti vyao...
Reply
Mallaba (Dk. Mallaba),
Reply
13/02/2010 3:31am
Hawa wanaandamwa kwa vile wamefoji vyeti na wengine kumbukumbu zinaonyesha kwamba hawakusoma kabisa. Baadhi yao pia waliwahi kutajwa hapa:
Reply
Mallaba 14/02/2010 8:19pm
Wahenga walisema elimu ni chanzo cha maarifa, on contrary to that also if the Education will be used inappropriately will be the source of disaster such as corruption,underdevelopment,lack of sustainable and better health services,decline in education system and an increase in the government dependence from donor contries e.t.c
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed