Hukumu ya Nguza Viking (Babu Seya) na Wanae 11/02/2010
Unaweza kuona video fupi ya kilichojiri baada ya hukumu ipo katika ukurasa wa video (bofya hapa) Vilio simanzi vilitawala leo katika viwanja vya Mahakama ya Rufani baada ya Msajili wa Mahakama hiyo, Jaji Neema Chusi kutangaza kuwaachia huru watoto wa mwanamuzi nguli, Nguza Viking 'Babu Seya' kwa kile kilichosemwa kuwa walifungwa kimakosa. Hukumu hiyo imeanza kusomwa leo saa 3 asubuhi, ambapo umati mkubwa wa wanamuziki kutoka bendi mbalimbali ndugu na jamaa wakifurika kufuatilia hukumu hiyo iliyokuwa ikisomwa kwa umakini mkubwa. ![]() Familia ya Nguza Viking ktk Mahakama ya Rufaa Feb. 11, 2010 Jaji Chusi alianza kwa kuchambua kosa moja baada ya lingine walilokuwa wanakabiliana nalo wafungwa hao. Katika mashitaka ya kubaka Jaji Chusi alisema kuwa, jopo lililokuwa likisikiliza rufani hiyo limebaini kuwa, katika mashitaka 10 ya kubaka yaliyokuwa yakiwakabili wafungwa hao Francis Nguza na ndugu yake Johnson Nguza hawakuhusika nalo. Amesema kuwa ushahidi unaonesha wazi kuwa wakati makosa hayo yakitendeka mtoto mmoja alikuwa shuleni na mwenzake alikuwa ziarani mikoani. Amesema kuwa upande wa mashitaka katika Mahakama ya Kisutu haikufuata sheria juu ya ushahidi uliotolewa kama kosa la kubaka lililokuwepo mahakamani kwakuwa haikuwepo PF 3 toka Hospitali ya Mwananyamala kwa maelezo. Ameongeza kuwa japo ushahidi wa mshitakiwa una mapungufu lakini ushahidi uliotolewa na Dk.Pretoria Ngeloi alidai kuwa, baadhi ya watoto walikutwa na maambukizi ya ugonjwa gono. Alisema kuwa ushahidi unaotolewa pande zote mbili ziridhike na nani kati ya washitakiwa alihusika kwa makosa ya kubaka na kulawiti. Ameongeza kuwa hivyo majaji wameona kuwa katika mashitaka hayo Babu Seya na Papii Kocha waliyatenda. Akielezea zaidi kuhusu mashitaka 11 ya kulawiti jaji Chusi amesema kuwa, wamebaini kuwa wafungwa hao wote hawakutenda makosa hayo bali kesi hiyo ilitungwa kwa nia ya kuwakandamiza. Kutokana na rufani hiyo Babu Seya na wanae walianza kuangua vilio hali iliyosababisha ndugu, jamaa na watu waliofurika mahakamani hapo kuanza kuangua vilio. Wakati wakiondoka kwenda Magareza Papii alionekana akiwa hana nguvu jambo lililofanya baba yake amsaidie huku askari wa Jeshi la Magereza wakiwa wameimarisha ulinzi. Mwandishi wa gazeti la DarLeo alipata fursa ya kuongea na ndugu na jamaa ambao walikuwa na maoni tofauti kuhusiana na rufani hiyo. Wakizungumza na gazeti DarLeo huku wakibubujikwa na machozi walidai kuwa, endapo Mahakama imeona kuwa watoto hao wawili hawakuhusika katika mashitaka hayo pia inaonesha hata hao wengine watakuwa wamesingiziwa. Wamesema kuwa kama mashitaka ya kulawiti wameondolewa washitakiwa wote baada ya kuona kuwa lilitengenezwa basi ni dhahiri hata hilo la kubaka nalo limeundwa. Ndugu wanaomba kama mashitaka yanaonekana yametengenezwa inaonesha na yaliyowatia hatiani pia yameundwa. Wanaiomba Serikali iangalie upya. Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Rufani baada ya jopo la majaji Salum Masati, Nathaniel Kimaro na Mbarouk Mbarouk kusikiliza rufani hiyo na kuichambua kwa kina hoja za mawakili wa akina Babu Seya iliyokatwa Novemba 30, mwaka jana. Wakili aliyekuwa akiwatetea awali, Herbert Nyange aliwasilisha sababu 15 za rufani kupinga hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa rufani hiyo, Marando aliongeza sababu nyingine nne za rufani hiyo. Kati ya sababu hizo alidai kuwa hakimu hakutenda haki wakati wa kusikiliza kesi hiyo kwa kuegemea zaidi kwa upande wa mashtaka na kuusahau upande wa washtakiwa. Pia Marando alidai kuwa mara kwa mara hakimu huyo alikuwa akipuuza ushahidi wa upande wa utetezi, pamoja na utetezi binafsi wa washtakiwa. Babu Seya na wanawe Papii Nguza 'Papii Kocha, Nguza Mbangu na Francis Nguza mwishoni mwa mwaka jana walikata rufaa kuhusiana na hukumu ya kifungo cha maisha jela iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Kisutu Addy Lyamuya. Pia mawakili wanaowatetea wafungwa hao waliiomba mahakama iwachie huru wanamuziki hao kwa kuwa hukumu iliyowatia hatiani ilikuwa na dosari nyingi za kisheria. Pia walidai kuwa kesi hiyo ilikuwa ya kupangwa na kwamba hawajawahi kuona hukumu ya hovyo ya aina hiyo tangu waanze kufanyakazi ya uwakili kwa zaidi ya miaka 30 sasa. Katika kesi ya msingi wasanii hao walikuwa wakituhumiwa kutenda makosa kumi ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya Aprili na Oktoba mwaka 2003 maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam. Habari kwa mujibu wa Na Rachel Balama, Mahakama ya Rufani wa gazeti DarLeo Commentsmkaazi 11/02/2010 3:29am
Nnji hii ngumu sana amini usiamini!!!
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed