![]() Hivi kwanini sisi wabongo tunapenda sana kufanyiana roho mbaya, ntimanyongo, ubangaizaji na short cuts? Wengi wetu hatupo honest... ukimpelekea fundi kitu atakulipulia ili mradi urudi tena... mwingine anaweza kukubadilishia kifaa akakupachikia kibovu akaondoa chako kizima... Ukienda kununua kitu unauziwa kwa kuangaliwa sura kwanza mimi nitaambiwa buku mbili, Supika kwa sababu kakaakaa kama Mzulu atapigwa kilo nzima... kitu kimoja bei tofauti kulingana na mtu... Ukijenga Uswahilini na nyumba yako ndo pekee ikawa na bomba la maji basi uwe mvumilivu kwa majirani... wengine wanaweza kukuamsha saa sita eti anataka kuchota maji... Ukipanga uswahili ukawa na ka-home thieta kako weka grill manake vibaka lazima waje kukutembelea... Una saa nzuri mkononi huna amani ukikatiza Magomeni mateja wanaweza kukufanyia kitu mbaya... Kwa walio ughaibuni unatuma pesa nyumbani ujengewe sahau hakuna cha tofali wala vumbi la kokoto litakalonunuliwa... Ukiharibikiwa na gari unaomba msaada wa kusukumwa kidogo lazima uwe na senti senti za kutoa... Ukipotea njia ili uelekezwe unaulizwa una hela? Nina barua ndogo ninahitaji bosi anisainie tu, utazungushwa wee na Sekretari wake mpaka utakata tamaa, kisa anajua ikisainiwa utapata mshiko, ukitaka umuone kwa chai kidogo... Unadai pesa za malimbikizo bosi anakuzungusha tu makusudi ili usiipate pesa yako au ukate tamaa kufuatilia wakati pesa haitoki mfukoni mwake. Hizi roho mbaya sijui zinatoka wapi? Kwa nini tupo hivi sisi? Mpaka tutwangane bakora? Yaani watu hawawezi kuwa honest japo kidogo? Yaani tabu tabu tabu... ah bubu husema... Monsignor, China CommentsBahati 01/03/2010 2:53pm
Hizo tabia ndio zinatutia umasikini na aibu, Kwasababu kila kitu mtu anaweka usanii. Haki ya mtu apewe bila kutoa chochote.Lakini Kwa TZ haiwezekani, unahitaji kununua kiwanja ujenge nyumba, lakini utazungushwa na HArmashauri husika mara nenda Wizara ya Ardhi mara tunapima miaka inakwenda na watu wanazidi kujenga kwenye maeneo Kiholela. Bora Magufuri aridi Wizara ya Ardhi.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed