Leo ni kumbukumbu ya vita ya Maji Maji 27/02/2010
![]() Leo ni kilele cha maonesho ya kumbukumbu ya vita ya Maji Maji yanayofanyika kila mwaka mkoani Ruvuma. Kutokana na umuhimu wake katika historia ya ukombozi wa taifa la Tanzania, mwaka huu, maonesho hayo yamepewa hadhi ya kuwa mojawapo ya makumbusho ya kitaifa na mji wa Songea kuwa na hadhi ya mji wa kihistoria. Historia fupi ya vita ya Maji Maji (kadiri ya kumbukumbu ya simulizi la mwalimu wangu wa shule ya msingi Mkolowony) Vita ya Maji Maji ilijipatia jina hilo kutokana na imani waliyokuwa nayo wapiganaji na wananchi waliyopewa na mganga ya kuwa, kwa kujipaka dawa ya maji maji katika vita ya kuung'oa utawala wa Mkoloni ingesababisha risasi za Wajerumani kuyeyuka na kuwa maji bila kuwadhuru. Vita hiyo ilianza mnamo mwaka 1905 ikiongozwa na Chifu Chabruma wa Wangoni ikianzia katika eneo la Lumecha, umbali wa maili kumi toka kwenye Boma ya Mjerumani. Mnamo mwezi Juni mwaka 1906, chifu Chabruma alijeruhiwa vibaya na ilimbidi kuvuka mto Ruvuma na kuingia katika utawala wa Wareno ili kujipatia hifadhi katika lindo la Chifu Mataka wa Wayao. Baada ya kupata ahueni, chifu Chabruma aliazimia kuendelea na mapambano ya kumng'oa Mjerumani, lakini azma yake haikutimia, kwani alifikwa na mauti kwa kuuawa na aliyejifanya kuwa mrithi wake. Vita hiyo ilikoma mnano mwaka 1907. Inakadiriwa kuwa watu waliopoteza uhai katika vita ya Maji Maji ni kati ya 120,000 na 135,000. Mungu azilaze pema roho za mashujaa wazee wetu. Pichani ni Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein na ujumbe uliofuatana naye wakitizama sehemu iliyotumika kunyongea Machifu wa mji wa Songea katika karne ya kumi na tisa. Picha kwa hisani ya blogu ya Mzee wa Mshitu - Yahya Charahani Commentsyasinta 27/02/2010 7:33am
Da Subi ! asante kwa kutumbukumba kumbukumbu hii ya kihistoria. mwaka jana nilikuwa kule.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed