Picture
David Mathayo David
Gazeti la Nipashe linaripoti kuwa baadhi ya Mawaziri, Naibu Mawaziri na Wabunge wanaodaiwa kuwa mafisadi wa elimu, hawajapeleka vyeti vyao katika Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kwa ajili ya uhakiki. Mkurugenzi Mtendaji wa TCU, Profesa Mayunga Nkunya, alisema hadi jana ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk. David Mathayo David, ndiye aliyekuwa amewasilisha vyeti vyake ambavyo vimethibitisha kuwa ana fani alizosomea.

Naye mwanaharakati Kainerugaba Msemakweli amesema hujuma dhidi ya harakati za kupambana na ‘ufisadi wa elimu nchini’, unaodaiwa kufanywa na baadhi ya vigogo nchini, zimepamba moto, baada ya mpango wake wa kuanika zaidi kashfa hiyo kupitia mabango kukwamishwa. “Nimehujumiwa. Maana tarehe 18 (mwezi huu) watu wanne walikwenda kampuni ya mabango na kuwatisha kuwa wakikubali niweke mabango watachunguzwa kodi zao na mabango na wamejenga kwenye hifadhi za barabara. Naandaa kuwafungulia kesi kwa kuvunja mkataba na mimi”.

Mabango hayo ilikuwa yawekwe katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na kwenye majimbo yanayowakilishwa na wanasiasa hao, ikiwa ni hatua ya tatu ya mapambano aliyoyaanzisha dhidi ya ufisadi wa elimu nchini. Jijini Dar es Salaam yangewekwa katika daraja la Salender, Jangwani, makutano ya barabara za Nyerere na Kawawa na Barabara ya Kilwa karibu na bandarini.

Kabla ya hujuma dhidi ya mabango hayo, Msemakweli alilalamikia kufanyiwa hujuma vitabu alivyochapisha vinavyoelezea kashfa ya vigogo hao jijini Dar es Salaam na mkoani Mwanza, ambapo mtu mmoja alionekana akinunua nakala zaidi ya 600 kwa mkupuo mmoja bila kujulikana anakozipeleka.

Kwa habari kamili, jisomee gazeti tando la NIPASHE kwa kubofya hapa

 


Comments

Ernest
01/03/2010 04:25

The Wavuti Administrator, could you please find out about this Mwingira of the Efatha Ministry at Mwenge, Dar es Salaam on serious allegations that he has demolished and destroyed properties of investors at the same site recently worth billions of Tshs. He is supposed to appear in court to answer these charges. Conduct your espionage and info us. Thankx.

Reply
Mkali Mani
12/03/2010 10:22

TCU hawajafanya kazi nzuri, cheti hakimaanishi kwamba mtu amesoma kilichoandikwa humo. TCU wanatakiwa kupiga simu hivyo vyuo na kuuliza hizo idara husika kama kweli huyo mtu alisoma hapo. Pia tuhuma za kughushi PhD ni kubwa sana, PhD haihakikishwi kwa cheti, wapo watu wengi wana PhD bila cheti. TCU watatakiwa wafuatilie huyo mtu ameandika thesis ya ukweli au hicho cheti kakinunua huko Free State. Kazi ya kuhakikisha bado, vigogo wanatumia ujanja wa aina mbali mbali. Hata mimi naweza kutengeneza cheti cha PhD cha UDSM au hata Harvard. Kupiga simu na kutoa ushahidi wa kutosha ndivyo vitakavyomsafisha huyo waziri feki.

Reply
Selemani
16/03/2010 04:42

Matayo David Msuya nimekuwa naye tokea high school Tosamaganga Iringa, akifanya CBG 1989-91, tukiishi bweni la Mwenge. Tulimaliza wote high school na Matayo alifaulu vizuri sana alipata daraja la kwanza point 7. Si kwamba alikuwa kifaru sana darasani, Matayo alisaidiwa na kaka yake aliyekuwa aakifundisha Mkwawa teachers college, nakumbuka usiku ule Matayo alipotea kwenye premises za Tosamaganga, na alikuwa alitokea mjini na kuingia kwenye mtihani Matayo aliiba mtihani na kufaulu sana masomo ya Chemistry na Biology kinyume na uwezo wake darasani. Tulikwenda na Matayo JKT itende, Mbeya. Kwa kuwa mwenzetu alikuwa amefaulu sana kuliko sisi watoto wa masikini ambao hatukuweza kuiba ama kuchangia mtihani ule. Matayo alichanguliwa kwenda kusoma Makelele Uganda kwa kupitia mfuko wa mwalimu Nyerere, ambao ulikuwa unsomesha wanafunzi walifanya vizuri. Ajabu, Matayo alichukua zile pesa na hakwenda Uganda, akaamua kusoma Sokoine University degree ya tiba ya mifugo (Bachelor of Veterinary Medicine) mwaka 1993-1997. Matayo alikuwa ni mwanafunzi pekee aliyekuwa na radio yenye double deck, (system) na TV set. Aliweza kununua hivyo kwa pesa aliyotakiwa kusomea Uganda. Kwa kuwa alikuwa na double scholarship ile ya Elimu ya juu ya Tanzania na ile ya Mwalimu Nyerere alikuwa na pesa sana aliweza kuchukua wasichana wazuri wote pale chuoni ikiwa ni pamoja na Mugros. Nakumbuka aliachana na Betty Manase kwasababu Matayo alifumaniwa akiwa na msichana mwingine wa kijijini, na Mathayo alipigwa kibuyu. Siasa alizianza rasmi mwaka 1995 alitumia TV yake kwenda kuonyesha vijijini madhara ya vyama vingi, alitumia mapigano ya Rwanda na Burundi kama kutishia wananchi wasikubali upinzani na kipindi kile wananchi walikuwa wepesi kuelewa kumbuka TV hazikuwa nyingi Tanzania kipindi kile. Alijijengea umaarufu sana ndani ya chama mkoani Morogoro na kitaifa. Aligombea ujumbe wa NEC mkoa wa Morogoro kundi la vijana alishinda. Matayo alimaliza SUA 1997 na kupata kazi ya kufundisha chuo kimoja Botswana. Kwa kuwa mjumbe wa NEC alikuwa karibu na akina Lowasa, JK na vingunge wengine aliweza kuwa anaonana na akina Makamba na akawa ni mwanamtandao. Matayo mwaka 1997 alifanya usanii wa hali ya juu alichangisha wanafunzi wa miaka ya mwisho Shs 10,000/= ilikupata form za kutafutiwa kazi Botswana alikusanya zaidi ya Tshs million 2,000,000 ambazo alitumia kununulia gari. Hahahahah…Pia Dr Matayo alirudi Tanzania na kudanganya wanafunzi wa SUA na kwa kutumia mabasi ya Aboud alipeka zaidi ya wanafunzi 200 Dodoma kupokea kadi za sisiem chini ya mwenyekiti wa CCM Mkapa. Wanafunzi walidanganya wangepatiwa ajira….hii ilimjenga sana Matayo na aliisha kuwa amekuwa maarufu kwenye ofisi za chama Dodoma, kama mjumbe wa NEC na mkutano mkuu..Pia alikuwa ameisha wadanganya akina Mkapa na wanamtandao wengine kuwa ana PhD. Mwaka 2000 aligombea Ubunge Same Magharibi na kushinda na kuteuliwa kuwa waziri mdogo. Ninamvyomfahamu Matayo ameweza kuapanda chat sana kwa kutumia usanii, 1997-2001 inaonyesha ameweza kusoma MSc 2 na postgraduate diploma moja na kumalizia PhD (Agriculture). Jamani mimi hii ilinisumbua sana nilibahatika onana na Prof Msolla wakati huo alikuwa waziri wa elimu ya juu na sayansi ambaye alitufundisha wote na anamjua vizuri Matayo, nilimuuliza Mh Msolla vipi kuna wabunge wenye vyeti vya kuforge ama kununua, na mnukuu prof Msolla, “Biungeni na kwenye serikali kuna viongozi wengi wenye vyeti vya kugushi, naliisha mwita Dr Matayo kumuuliza PhD alifanya lini na wapi na pia aniletee PhD thesis yake, Matayo aliogopa sana na alikili mbele yangu, kuwa Prof mimi nimetumia hii title kisiasa zaidi, sina MSc wala PhD” mwisho wa kunukuu, Msolla alisema amepeleka kwa raisi wale wote wenye vyeti vya kugushi aliweza taja majina, Dr Nagu, Dr Nchimbi, Dr Kamalla, Dr Matayo na wengine wanavyeti vya kugushi vya sekondari, shahada za kwanza na Msc. Challenge aliyokuwa nayo Mh Msolla ni kusumbili utekelezaji wa raisi maana yeye anasema hawezi mlazimisha raisi kuchukua uamauzi. Raisi alimshukuru sana Msolla akaahidi kulifanyia kazi lakini yuko kimya ….kazi sijui zikoje kule wizara ya kilimo Msolla na Matayo..kazi ipo ninamfahamu sana Matayo yuko tayari kufanya lolote apate madaraka ya kisiasa, na ni fisadi wa muda mrefu. Alikuwa akipokea mishahara miwili ya uwaziri na ile kazi alokuwa akifanya Botswana huyo ndiye Mh Matayo David Msuya Matayo.

Reply
mnene
22/03/2010 17:48

E bana eeh changa la macho tayari. Ndo maana Mtikila alisema watanganyika wote makondoo.

Reply



Leave a Reply