Habari za kusikitisha toka kijijini Ibaraizibu wilayani Bukoba katika mkoa wa Kagera zinasema kuwa Evance Rwelamira (miaka 25) amefariki baada ya kujinyonga kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni baada ya kufeli mtihani kwa mara tatu mfululizo. Taarifa za sababu ya kifo hicho zimetolewa na ndugu wa marehemu, bwana Device Rwelamira ingawaje marehemu hakuacha ujumbe wowote kuhusu sababu ya kuondoa uhai wake. Kamanda wa polisi mkoani Kagera Bw. Henry Salewi alithibitisha kifo hicho alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kwamba mwili wa marehemu huyo ulikutwa ukining'inia juu ya mti. WAZO PEVU ni... Ni kweli kuwa msongo wa mawazo, kukata tamaa na kukosa msaada wa kisaikolojia huweza kkuchangia kwa kiasi kikubwa kupata hisia za kujiua ili kujitahidi kuepukana na kadhia hiyo. Baadhi ya shule huwa na Walimu Washauri ambao mbali na kazi yao ya kufundisha, pia huchukua nafasi ya ulezi na kuwa watu wa karibu, washauri na waelekezi kwa wanafunzi, hasa wanafunzi wanaoonekana kusumbuliwa zaidi na masuala ya masomo au masuala binafsi ambayo ni vigumu kupata utatuzi katika familia. Baadhi ya wanafunzi pia huhitaji msaada zaidi hivyo huonwa na wahudumu wa afya wanaofanya kazi ya ushauri nasaha na saikolojia ambao husaidia kukabiliana na hali ngumu na msongo wa kiakili na kimawazo. Kwa kweli tunahitaji walimu wenye kuweza kutoa ushauri elekezi kwa wanafunzi. Ili kuwapata walimu hawa, tunahitaji Wizara husika kujali maslahi ya Walimu ili nao waweze kuwajali Wanafunzi. CommentsMallaba 11/02/2010 1:30am
jamani kama mtu hujawahi kufeli mtihani ..sikia tu wala usione..
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed