![]() Hawa wageni wa Kiswahili walinishangaza sana majuzi nilipokuwa naperuzi picha katika tovuti ya kuhifadhia picha ya Flickr. Basi aliyezibebesha picha zenye maneno yenye tafsiri ya lugha kadha wa kadha, mojawapo ilikuwa ni ile iliyopewa jina Swahili inasomeka, 'VITA NI JUU KAMA UNATAKA IT' (pichani kushoto). 'asa mi n'kajiuliza, ala, huyu alitaka kusemaje? na maana yake ipi? Katika kudadisi ndipo nikasoma alichoandika kwa lugha ya Kiingereza, 'WAR IS OVER IF YOU WANT IT'. Nikagundua hapa imetumika tafsiri ya neno moja baada ya jingine ama kwa kutumia kamusi au mashine ya "google translate" ambapo: WAR = VITA IS = NI OVER = JUU IF = KAMA YOU WANT = UNATAKA Ndo matokeo yake wakapata hii kanyaboya. Hawakufahamu kuwa kuwa neno moja laweza kuwa na maana zaidi ya moja au matumizi ya neno yaweza yasilete au yapoteze kabisa maana kulingana na ujumbe unaokusudiwa kufikishwa. Kumbe walipaswa kuandika, 'VITA IMEKWISHA...' Sasa basi ndiyo hata nikajikumbusha, ya kuwa, ukitaka kujifunza lugha ngeni, shurti uulize wenyeji, la umekwama, akheri ukaingia darasani kabisaa, usijeleta shari katika lugha ya watu ukaonwa kituko buree. Comments04/02/2010 7:57pm
Njia bora ya kujifunza lugha ngeni ni kwenda huko huko inakosemwa ukaishi na waisemao na kujifunza utamaduni wao. Wakati mwingine hata kujifunza darasani tu haitoshi.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |






RSS Feed