Nukuu ya leo toka kwa Watanzania 11/02/2010
![]() ...kuna wanabidii, wanakijiji, wapiganaji, wanamapinduzi etc. Usisahau, hawa wote ni Watanzania wanapaza sauti, wanataka maisha bora! Oh Lord, hear us! - BaMbo, Botswana. Graciously hear Us! - Monsignor, China. ![]() Nyie msijali, mkufuruni Mungu tu kwa kumchagua kaka Chenji, Mlamba Rombo, Low-A-Sir Manduli na kule Bookoba msimuache Kaa-la-Maji pia na huku na huko wachagueni tu. Mnayajua mabaya yao yote ila wachagueni tu hata kwa kanga na tisheti tu. Wala msijali Mungu atawasikia tu; japo kawapa akili na hamtaki kuzitumia sasa mnalia tu. Chagueni mafisadi kisha msubiri uokovu wa Mungu tu. Wala msijali. - Mpiga Paka, Tanzania. ![]() Mpiga Paka, hilo nalo neno...Watanzania wanalalamika maisha magumu, na kweli wamechapika, wanatia huruma, wamejikondea, mama zao wanakufa wakati wa uzazi, watoto wana unyafuzi, wenyewe wanakufa kwa njaa, watoto wakifaulu wakaenda kwenye shule za kata wanapata div sufuri, mahospitalini hamna dawa, barabara hazipitiki, hata ile reli ya mkoloni ilishaharibika, kila kitu kiko hoi, na mchawi wao wanamjua, amekuwepo nao miaka nenda rudi, wanamjua ila hawataki kumuondoa, wanafikiri malaika atatoka Mbinguni kuwabadilishia hali yao, wanaamini hamna mwingine awezae kubadili hali yao isipokua aliyepo... ndo hao ndugu zao wa Bahariadi, Manduli, Bookoba, Rambo, na kwingineko... unafikiri hawaoni? ...wanaona sana, na ndo maana watawarudisha mjengoni kwa vema nyingi (daftari litajaa pata, vema)... kisha wataanza tena kulalamika... watapaza sauti kuilalamikia Serekale, ambayo wameiweka madarakani kihalali...we subiri, si utaona?! - LeBron, Japan. CommentsMonsignor, China 11/02/2010 6:31am
LeBron, Kiva nimewasoma. Nakubali tatizo ni wananchi wenyewe ama kwa kutokujua ni kipi wanakihitaji au kwa kuridhika na hali iliyopo. Bado wananchi wengi wamelala na wameridhika na hii hali ya kulala na kutohitaji mabadiliko. Nguvu ya wanasiasa wachache wanaohitaji mabadiliko haiwezi kufanikiwa bila backup kuwa na wananchi wengi wenye kuhitaji mabadiliko. Kwahivi tutaendelea kupiga kelele lakini wale wanaopigiwa kelele kwa manufaa yao wamejiridhisha na hii hali na wala hawaoneshi kushtuka kuhitaji mabadiliko haya kwa sasa. La muhimu ni kuwaamsha hawa waliolala waone kinachopigiwa kelele ni kipi ili washtuke nao wadai mabadiliko.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |







RSS Feed