Simba yageuza wembe upande wa pili 09/02/2010
Baada ya kuwekewa kauzibe huko nyanda za kanda ya ziwa Nyanza, hatimaye leo timu ya Simba Sports Club wamegeuza makali ya kiwembe upande wa pili na kuwanyoa Manyema Rangers FC mara mbili. Ilikuwa ni dakika ya 63 mchezaji wa simba Ulimboka Mwakingwe alipoiandikia Simba bao lake la kwanza. Bao la pili liliwekwa kimyani kwa njia ya penati kunako dakika ya 71 baada ya wachezaji wa Manyema kumfanyia 'ndivyo sivyo' mchezaji wa Simba Mussa Hassan 'Mgosi' katika eneo la hatari na hivyo kuzaa penati hiyo aliyoifunga mwenyewe 'Mgosi'. Mechi ilichezwa katika uwanja wa Uhuru. Hadi mwisho wa mechi ni Simba SC 2 Manyema Rangers FC 0. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed