Posti iliyotangulia nimeandika namna ya kupata matokeo ya kidato cha nne. BOFYA HAPA kusoma. Nimeshindwa kuvumilia, acheni tu leo niseme, nimeshikwa na hasira ni vile nimekosa viwembe na chupa za kutosha za kujimaliza. Nitatafuta sumu ya panya baadaye nikishamaliza kumwaga hasira zangu leo. Nasema wizara ya Elimu na vitengo husika hasa cha IT na mambo ya tovuti mnatia aibu, mnakera na kuchefua. Nasema hivi kutokana na usumbufu ambao wahitimu wa kidato cha nne na sita wamekuwa wakiupata kila msimu wa matokeo unapowadia. Leo najivisha cheo cha kuwasemea wadogo zangu hawa. Iko hivi: Kila matokeo yanapotangazwa kuwa yametoka rasmi, vijana wamekuwa wakijituma kwenda Wizarani; punde wanapofika huko hutakiwa kupunguza msongamano na kuelekezwa kwenda mashuleni ambako nakala za vitabu vyenye matokeo hayo vimewekwa. Huko kwenye mashule nako ni usumbufu ule ule. Mara mwalimu husika na vilipo vitabu hivyo haonekani. Mara ofisi yenye vitabu haijafunguliwa. Mara mwalimu ana shughuli maalumu subirini. Alimradi tu watapewa vijisababu mia kidogo wakitakiwa kusubiri pasina kujua wasubiri hadi muda gani. Hivi lengo lenu kuwafanyia hivyo ni kuwakatisha tamaa au mnadhani kwa kufanya hivyo mnakwepa usumbufu? Kwa taarifa yenu tamaa hawakati wala usumbufu hauondoki msipowaonesha matokeo; zaidi sana mnawatia hasira tu za bure, bure kabisa! Mtu mwenye akili timamu lazima ajifunze kuona mbele kuwa mtu uwapo katika hali ya uhitaji iliyo na simile ndogo (desperation) ni rahisi kupandwa jazba (to be provoked) kutokana na kunyimwa iliyo haki yako. Hili likitokea bila shaka tutasikia katika vyombo vya habari wahusika wakisema wanafunzi si wastaarabu na wavumilivu. Nashindwa kuelewa wahusika hao wanashindwa vipi kukumbuka saikolojia ya vijana? Lau hawana elimu ya saikolojia hiyo, japo wakumbuke wao wakiwa katika umri huo walikuwa wakijisikia vipi wanapohangaishwa na majibu yao? ule mchecheto walikuwa wanauzima vipi? wao wanadani vijana wa sasa hawana mchecheto? Historia ya tatizo: Kwa mara ya kwanza kusoma vilio hivi ni wakati wahitimu wakitafuta matokeo ya mtihani wa mwaka 2007. Tukajipa moyo kuwa kwa bahati mbaya huenda maji yamezidi unga, si neno, tusubiri mwakani. Mwaka ulofuatia kelele ilikuwa ni ile ile na pengine kuzidi. Tena mwaka huu 2009! Jamani eeh, imezidi hii. Miaka mitatu (2007, 2008, 209) mfululizo tatizo ni lile lile, ina maana kuwa hamsikii au hamtilii maanani kadhia hii mnayosababishia vijana wetu? Yaani ni kweli kuwa Wizara imeshindwa kutenga fungu la kununua bandwidth kubwa kwa wizara hii nyeti ya Elimu ili kukidhi mahitaji ya muda huu mfupi? Isisingiziwe gharama au hasara hapa jama. Sioni hasara yoyote kwani bandwidth itakayotumika ni maalumu kwa kipindi kifupi tu lakini muhimu sana hivyo inaweza kulipiwa kwa kipindi fulani tu. Naomba mtu asiniongopee kuwa haliwezekani kwani ninafahamu, tena si kufahamu tu, ninajua kuwa inawezekana. Tatizo lililopo ni la wahusika kutokutaka kuuliza na kupata maoni ya kipi cha kufanya. Wahenga walisema kuuliza si ujinga, na asiyeuliza hanalo ajifunzalo. Enyi wahusika wa kigengo hiki, kila leo mambo hubadilika; ulilojifunza jana leo laweza kuwa halifai, elimu ya usiku yaweza kuwa kiporo cha asubuhi, tena katika ulimwengu huu wa teknolojia ambapo kila leo zinazaliwa scripts na codes mpya. Tafadhali muache 'kujiona' na mkubali kupatiwa ushauri na kuufanyia kazi ule unaofaa. Suluhisho ama pendekezo langu? Mi nadhani suluhisho mojawapo ni kwenu ninyi wahusika wa IT kuwa elekezeni maswali yenu kwenye kundi la eThinkTankTz (eTTTz) kwani ninayo imani kubwa kuwa mtapatiwa ufumbuzi kutoka kwa wataalamu wengi wanachama wa kundi hili. Nafahamu mnaifahamu eTTz, ila ni 'ego' yenu imekuwa kubwa kuliko masilahi yetu tulio wengi. Linki yake ni www.ethinktanktz.org. Humo wapo watu ambao wamejitolea kabisa ku-host tovuti hii bila malipo yoyote ili tu kuondoa kadhia hii. Ninajua Wizara itajitetea kuwa ni chombo cha Serikali hivyo mtu binafsi au shirika lisio la kiserikali haliwezi kupewa ruhusa ya kufanya hivyo; ikiwa huo ndiyo utetezi na taratibu za kiserikali, basi tupatieni tovuti inayofanya kazi hasa katika kipindi inachohitajika kuliko wakati mwingine wowote. Nimekasirika? Ndiyo! Tena sana tu! Ni aibu na inakera! Ninyi watu kweli mfikage mahali muondoe 'ego' zenu zilizojaa maringo mbuzi na mvae utu na maslahi ya wote mbele. Yaani mi nachukiaga! Sasa nimesema sana, naweza kwenda kutafuta ile sumu ya panya ninywe.... Loh! Thubutu yake. Hanywi mtu sumu wala nini hapa. Ttutapambana na kero hizi hadi liamba walahi. Ala! CommentsBlogger Sun, 07 Feb 2010 7:26:50 pm Mbona nimefungua tovuti na sioni tatizo. Speed ya tovuti yao siyo mbaya. BLOGGER Sun, 07 Feb 2010 9:10:51 pm Kaka, site yao haina tatizo na wala tovuti yao haina shida, naona speed ni normal kwangu mimi, hata hivyo connection speed yangu ni Broadband 5.0 Mbps (Megabites per second), Hivyo nadhani tatizo ni tofuti yako! au bado unatumia dial-up connection badala ya broadband? Blogger Sun, 07 Feb 2010 9:13:55 pm ... Sorry i meant 54.0 Mbps not 5.0..... David Mon, 08 Feb 2010 2:17:44 am Huyu aliyeandika kuhusu tovuti ya baraza la mitihani amechanganikiwa.Tovuti ya baraza ni www.necta.go.tz.Inapatikana muda wote popote pale ulipo.Namshauri kabla ya kubwatuka afanye utafiti wa kutosha badala ya kuongea pumba. David Mon, 08 Feb 2010 2:44:05 am mtandao kwa ajili ya ku download information katika kompyuta yako. David Mon, 08 Feb 2010 2:47:04 am Downlink speed ni speed ya mtandao kwa ajili ya ku download information katika kompyuta yako. Mon, 08 Feb 2010 9:59:16 am David, emmanuel samwel Mon, 08 Feb 2010 10:10:19 pm huyo chalii ni soro tu hana jipya katika ulimwengu wa u tandawazi hilo si tatizo la necta bali watu watumiao mtandao ni wengi mno na wote wana tumia kwa wakati mmoja hivyo mtandao unakuwa overloaded. Hivyo basi siku nyingine ajipange asipanick tu afikiri kwanza David Mon, 08 Feb 2010 10:19:59 pm Bora useme wewe Emmanuel. Comments are closed. |