Ukitizama video ya wimbo wa mwanamuziki Akon wa Oh Africa alioutunga mahsusi kwa ajili ya kombe la Dunia la mpira wa miguu Afrika Kusini 2010, utaziona rangi za bendera ya Taifa la Tanzania. Zifuatazo hapa ni picha nilizokamata toka kwenye video hiyo ambayo unaweza kuisikiliza kwenye ukurasa wa videos (bofya hapa) au kusikiliza audio kwenye ukurasa wa audios (bofya hapa). Ni katika kutizama wimbo huo nimejiuliza ikiwa wahusika wa Utalii Tanzania wanaweza kuipa kipaumbele (promotion) video hii ili kujipatia sifa ya kuitangaza nchi kwa bendera inayoonekana humo. Isije ikawa tuna'omba Mungu' siku tu Akon ashukiwe na Malaika akurupuke atutungie tangazo atuletee aseme hili hapa kwa ajili yenu kuboresha utalii. Loh! kwa kupenda vya bwerere? huenda twashindwa bure. Nadhani ni fursa nzuri ya kutumia video hiyo yenye mahadhi ya Kiafrika kujipatia-ujiko (sifa) bure. Nataka kujiaminisha kuwa wapo wabunifu wa sekta ya utalii wanaoweza kuifanyia kazi hii na sidhani kama Akon atakataa ikiwa atatakwa ruhusa na ridhaa ya kutumia video hiyo. Tusiiwekee ukomo kwa kudhania kuwa haiwezekani, tujaribu kwa juhudi kwanza na tuache kupenda vya mreremko. Commentsanonymous 17/02/2010 7:31am
Watu wetu wa utalii hawako creative kiasi hicho. I do n't think if that will be possible. They are not serious! kama wewe ni mtazamaji wa CNN channel utakuwa umeliona tangazo linaloelezea Tanzania. Tangazo hili ni "too short" na halieleweki hata kwa sisi watanzania wenyewe, je asiye mtanzania atalielewa kweli?? Linganisha tangazo letu na lile la Angola ambalo ukiliangalia tu unapata picha halisi Angola ni nchi ya vipi na kuna nini. Hawaelewi kwamba matangazo kama haya yana mchango mkubwa sana katika suala zima la promotion ya nchi. Nasema tena, they are not serious!!!
Reply
paesulta 17/02/2010 10:45pm
Habari za kazi?
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |








RSS Feed