wavuti
wavuti logo Facebook icon Facebook icon Twitter icon Subscribe RSS
 
Kwa mara ya pili waigizaji nyota wa Kinigeria Chinedu Ikedieze aka Aki (29) na Osita Iheme aka Ukwa (28) wanatarajia kuwepo nchini Tanzania katika jiji la Dar Es Salaam tarehe ya 14 Februari 2010 kwa ajili ya tamasha la kuwachangia watoto yatima. Mara ya kwanza vijana hao walifika nchini Tanzania kuhudhuria uzinduzi wa filamu ya "Dilema".
Picture
Chinedu Ikedieze (Aki ) & Osita Iheme (Ukwa)
Wasanii hao, ambao siku zote huonekana kama watoto ingawa ni watu wazima, wamejizolea umaarufu nchini kutokana na vituko vyao wanavyoonyesha kwenye filamu mbalimbali za Kinigeria. Baadhi ya filamu hizo ni kama vile ‘Aki na Ukwa', 'Pipiro','Back to America', '2Rats', 'Secret Adventure', 'Mr Ibur' na nyinginezo.

Mkurugenzi wa asasi inayowaleta wasanii hao ya Education and Expedition Agency, Clemence Kambengwa, alisema wanawaleta wasanii hao ili waweze kushiriki katika uzinduzi wa tamasha la kila mwaka kwa ajili ya yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini. "Yatima na watoto waishio katika mazingira magumu wanastahili faraja… nasi tumeamua kuwaleta Aki na Ukwa ili washiriki uzinduzi wa tamasha hilo la kuwapa nguvu watoto na ambalo litakuwa likifanyika Februari 14 ya kila mwaka," alisema Kambengwa.

Akifafanua zaidi, Kambangwa alisema tamasha hilo litakalozinduliwa na wasanii Aki na Ukwa, litafanyika katika viwanja vya TTCL Kijitonyama na baada ya hapo, hakutakuwa na onyesho jingine la waigizaji hao. "Aki na Ukwa watashiriki tamasha la siku hiyo tu na baada ya hapo wataendelea na ratiba nyingine ambazo ni kutembelea mbuga za wanyama na kwenda kwenye Mlima Kilimanjaro, kwenda Mererani mkoani Manyara kwa ajili ya kutembelea migodi ya Tanzanite ambayo wamedai wanataka kuiona.

 


Comments


Comments are closed.