Eti we mwoga wa mende kama huyu? 03/03/2010
Humu duniani watu tunatofautiana kiwango cha ujasiri. Lakini wapo watu wengine japo wawe jasiri kiasi gani, ikiwa wana ugonjwa wa kuogopa, baadhi ya vitu (phobia) ujasiri wake ni kazi bure katika nyakati fulani. ![]() bofya pichani utizame video hii fupi Ninakumbuka nilpokiuwa Sekondari dada mmoja alikuwa mwoga sana wa wadudu kama vile sisimizi, nyenyele, maji ya moto nk. Mwanzoni nilidhani ni utani kwa kuwa umbo lake lilikuwa kubwa kuliko wanafunzi wengi, na hivyo tulitarajia mtu mkubwa asiweze kuogopa kidudu kidogo hata siku moja. Tena, nilipokuwa chuoni, nilisoma na dada mwingine ambaye ni rafiki yangu pia, naye alikuwa mwoga wa wadudu hasa aliyekuwa akimtikisa maini alikuwa mdudu mende. Halafu hivi vidudu bwana hata sijui vinakuwa vimetumwa na nani kwani hisia zao huwa ni kali na mara moja huwapeleka kwa yule mtu mwoga. Hii nadhani ni kutokana na msisimko (stimulation) zinazosababisha kemikali fulani kuzalishwa mwilini na mtu huyu baada ya kumwona mdudu au kiumbe anayemwogopa. Siku moja hivi tupo koridoni, nje ya milango ya vyumba vyetu ambavyo vilikuwa vinatenganishwa na uwazi wa kuelekea bafuni, alikuwa akijipita mende katika harakati zake za pengine kutafuta chakula. Ghafla, rafiki yangu ambaye kwa wakati huo alikuwa amesimama kati ya mlango wa chumba chao na kile cha kwetu huku akiukabili mlango wa bafuni, ghafla alipiga ukelele wa nguvu mara moja. Ndipo tulipostuka na kumwuliza, 'nini?' huku akinyoosha mkono akawa anasema, 'yule, yule', siye kumtizama ni mende, mimi mawazo yangu nilidhani kamwona nyoka ama ng'e ama pengine sijui kidudu gani cha kutisha. Loh, kumbe alikuwa akimwogopa mende. Alitetemeka, akamkamata mmoja wetu bila ya kumwachia akisema, 'mwue, mwue' nasi kwa kuwa tuliona kichekesho, hatukumwua, ndipo yule mende ghafla aligeuza akashika njia kuelekea upande alikokuwa amesimama yule dada muda wote akimshikilia mwenzie. Kuona vile, yule rafiki yetu huyu akaanza kujisogeza nyuma zaidi kadiri mende alivyomkaribia. Mende alipomkaribia kabisa yule dada aliyekuwa ameng'ang'aniwa, ndipo rafiki yetu alipiga hatua moja kuelekea nguzo iliyokuwa imeshikilia dari, la haula, mende anaye. Mende kama katumwa, akamfuata katika ile nguzo, ndipo rafiki yetu akapiga tena ukelele wa nguvu, 'nakufaaa...' Utaniuliza, 'kwa nini hakukimbilia chumbani kwake?'. Ni hivi, alishindwa kuwahi kuufungua mlango wake; vile vile, alitaka kuhakikisha kuwa mende anauawa ili apate amani kuwa hatamfuata chumbani kwake usiku. Ilibidi mmoja wetu amwue (sikumbuki alikuwa nani kati yetu) ili kuepusha watu kujaa na kutaka kujua kulikoni mtu 'anakufa' vile vile kutaka kuondoa ile aibu yakuwa dada fulani ni mwoga wa mende. Muda wote huo tulikuwa tunashikilia mbavu kwa kicheko (adabu zetu ndogo wakati huo, tunacheka msiba). Ilikuwa ni 'full' kuelewa somo la saikolojia ilipofika siku ya kufundishwa kipengele cha 'phobia' kwa maana kila mmoja aliikumbuka ile songombingo ya mende koridoni. Ndipo tulipong'amua kuwa alaa, kumbe ni ugonjwa. Na hapo ndipo nilipomkumbuka dada yuleee, wa Sekondari. Ama kwa hakika, usilolifahamu ni kama usiku wa kiza. Bofya hapa umtizame mtangazaji mmoja wa hali ya hewa akiteswa na mende studioni. Commentssui 04/03/2010 4:10am
anamaneno huyo!!!ata mende je sisinizi itakuaje???
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed