Picture
Issa Michuzi akikabidhi fulana kwa Hassan Abdulla mjini Reading
Habari kutoka kwenye blogu ya mwanabloga maarufu nchini, bwana Issa Michuzi 'ankal' au 'mzee wa libeneke' zinapasha kuwa, baada ya kuendeleza kazi ya kublogu kwa takriban miaka minne mfulilizo bila kuchoka, hatimaye fulana ya blogu ya jamii imechukuliwa rasmi kutoka kwa 'ankal' na kuwekwa pembeni tayari kwa kupigwa mnada ili kuchangisha pesa za maendeleo ya wadau.

Kampuni ya usafirishaji mizigo ya Hillview Family Company Limited ya mjini Reading, nchini Uingereza, imeinunua fulana hiyo kwa pauni 1,000 ili kuinadi na kuchangia mabloga kuendeleza 'libeneke' kwa ufanisi zaidi.

Siku ya mnada utaofanyika online itatajwa hivi karibuni, na mabloga wanaotaka kunufaika na 'libeneke la mnada wa ze fulanazzzz' wanatakiwa watume maombi ya msaada na anwani pepe zao kupitia issamichuzi@gmail.com ili kuweza kufikiriwa na jopo la blogu ya jamii na wataalamu wa Hillview Family Company.

Jumla ya mabloga wachanga 10 watanufaika na mpango huu ambapo watapatiwa laptops, modem za internet pamoja na pesa za hewani za internet ya miezi mitatu ili kuwawezesha kuanzia kazi. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 10 Aprili 2010. Mpango huu unamhusu bloga yeyote mchanga popote alipo duniani.

Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea www.issamichuzi.blogspot.com

Sisi wana wavuti.com tunatoa pongezi za dhati kwa Issa Michuzi na HillView Family Co LtD kwa kuweza kubuni na kutaka kufanikisha azma ya kuwasaidia wale wote wanaojitokeza kutaka kupasha habari kwa njia ya blogu. Ni matumaini yetu kuwa mpango huu utakuwa yenye manufaa.

 


Comments




Leave a Reply