wavuti
wavuti logo Facebook icon Facebook icon Twitter icon Subscribe RSS
 
Tunayo kila sababu ya kutoa pongezi nyingi sana kwa Hasheem Thabeet kwa kutia juhudi na kufuata maelekezo na kufanikiwa kurejea kwenye ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani (NBA).
Picture
Hasheem Thabeet
Hatimaye timu ya Memphis Grizzlies imemrejesha dimbani Hasheem Thabeet ambaye ni nyota wa Tanzania katika mchezo wa mpira wa kikapu, NBA, wa nchini Marekani.

Hasheem anarejea baada ya kuichezea timu ya Dakota kwa takriban wiki mbili katika ligi ya kujinoa al maaruf D-League. Habari zaidi za kwa nini alikwenda D-League unaweza kuzirejea kwa kubofya hapa.

"I was on the bench for a long time, I got to go out there and play big minutes, try to work on the stuff the coaches wanted me to do - rebound the ball, block shots, and be able to score when you get the ball. To stay active overall. I was successful doing that" - alisema Hasheem wakati akielezea sababu ya yeye  kuweko benchi muda mrefu na kutokuichezea Grizzlies michezo mitatu kati ya mitano  kabla ya kupelekwa Dakota.

Hivyo basi, lengo kuu la Hasheem kupelekwa D-League ilikuwa ni  kwa ajili ya kumpa changamoto, stamina na kujiamini zaidi ili aweze kukabiliana vilivyo katika michuano ya NBA. 

"They gave me a reason why I was going up there..., so it wasn't as tough as a lot of people were expecting. They explained to me why I was going there, and I was OK with it."

Akiwa na Dakota WIzards, aliichezea mechi sita na kufanikiwa kufikisha pointi nyingi zaidi  (19 ) siku ya Februari 28 na tarehe 5 Machi 2010 alifanikiwa kupata rebounds 18 na hivyo kuiwezesha Wizards kupata ushindi wa mechi 5-1 katika uwepo wake.

"He went down and played well," Memphis coach Lionel Hollins said. "He was a huge factor for them. The one game he fouled out, they lost in the end. They're not 5-1, if he's not blocking shots and rebounding the way he was, and even scoring."

Hii inadhihirisha kuwa kijana anaweza ikiwa anadhamiria.

 


Comments


Comments are closed.