Hongera Prof. Matondo kwa kuonesha mfano 02/03/2010
Mara nyingi tumezoea kusikia taarifa za kutisha na kusikitisha kama siyo kuhuzunisha kila linapotajwa suala la afya hasa katika zahanati, vituo vya afya, hosipitali za wiliaya, mkoa, rufaa na hata ile ya Taifa. Leo nimefurahi kuona habari yenye angalizo linalorekebika ila yenye moyo uliyojaa shukrani. Kwa hili, Profesa Matondo nakupongeza. ![]() Prof. Matondo Nzuzulima Mwaka 1993 nilifanyiwa upasuaji mkubwa wa sikio langu la kulia pale Muhimbili. Nakumbuka ilikuwa ni asubuhi majira ya saa mbili nilipopelekwa katika chumba cha upasuaji. Taa zinazong'ara sana zilikuwa zikiwaka na manesi walikuwa wanamaliziamalizia kuandaa vifaa.
Comments02/03/2010 2:09am
Kwanza napenda kukupongeza kwa kupata operation most succesful kulingana na sehemu ya eneo husika.
Reply
Vipi kitu 02/03/2010 3:12am
Very wrong,huwezi kumuelezea mgonjwa tatizo lake akiwa kwenye operating table, hii ni tabia mbaya ya kutoheshimu haki na privacy ya mgonjwa ambayo madaktari wengi wa Tz wanayo, hata kama ame conset bado wanafunzi hawatakiwi kujifunzia hapo bali walitakiwa zoezi kama hilo waende Darasani au Mortuary kwenye maiti zisizokuwa na wenyewe, kama ingekuwa ni mimi basi ningeidai Daktari na Muhimbili inilipe kwa kunifanya Guinea pig wao, hii inakuja jamani tubadilike
Reply
02/03/2010 8:00am
dk mallaba hebu tuelewane kidogo. shida tunayoipata sie maamuma wa udaktari ni kufundisha wanafunzi mgonjwa akiwa na fahamu zote. ndio maana ukisoma hili chapisho kwa muhusika mwenyewe, utakuta wamarekani walishangaa na kumuona kama mwanasesere.
Reply
02/03/2010 1:23pm
Mimi nadhani pengine mtafaruku huu ulitokana na mkanganyiko wa lugha. Kwa vile darasa lilikuwa linafanyika katika Kiingereza (tena kilichochangayika na ile misamiati kamambe ya kitiba), inawezekana Profesa Daktari Bingwa yule alidhani kwamba nilikuwa sifahamu Kiingereza (sawasawa) kama ilivyo kwa Watanzania wengi. Na kama nisingeweza kuielewa mada, basi kusingekuwa na tatizo lolote.
Reply
Vipi Kitu 03/03/2010 1:12am
Wengi wa madaktari na manesi hufanya makosa haya wakifikiri mgonjwa hajui lolote au kingereza ni cha kwao tu kumbe wanafanya makosa ya kitaaluma ambayo yanaweza kumghalimu hapo baadaye,ngoja nitoe mfano hai mmoja, Siku moja tukiwa ndani ya chumba cha upasuaji KCMC Hospital aliletwa mzee mmoja kufanyiwa upasuaji wa tumbo na hiyo ilikuwa mara ya saba au nane hivi, mee wa watu akiwa kapumzishwa akisubiri zamu yake kupanda kwenye meza ya upasuaji basi binti mmoja kati ya manesi akaanza kimombo chake kilicho changanyika na kikwao, akawa anaelezea wanafunzi kuwa mzee huyu anahisiwa kuwa ni HIV positive kwani ugonjwa wake umekuwa ukirudi kila mara, si munamuona hata alivyokonda, lazima atakuwa candidate etc, kumbe yule mzee alikuwa ni Regional Medical Officer mstaafu kama sikosei Iringa ndiko alikoachia kazi, kwa busara za yule mzee hakujibu kitu palepale lakini siku alipopewa discharge alimtumia salaam yule binti kuwa awe mwangalifu na mdomo wake kwani unaweza msababishia machungu huko mbeleni,hivyo basi utamaduni wa kufikiri tulivyozoea ni sawa si kweli inabidi wataalamu wetu wabadilike
Reply
Shukran za dhati zikufikieni Dk. Mallaba, Vipi Kitu, Bennet, John Mwaipopo na Masangu Matondo Nzuzulima kwa maoni endelevu na yanayotekelezeka kabisa kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu, viapo na miiko ya kazi. Jambo jema katika kusaidiana kutokuyarudia makosa ni katika kukosoa penye kosa na kisha kutoa ushauri, maoni au mapendekezo ya namna ambavyo jambo lapaswa lifanyike.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed