Jikinge na staili hii mpya ya wizi 13/03/2010
Kuna hili tukio la ukwapuaji wa kutumia gari ambao umekuwa ukishamiri sana hapa jijini kwa sasa,hivyo naomba uweke hapo mtaani kwetu ili wadau waweze kuwa makini na tukio kama hili. Kuna tukio limetokea hapa Sinza maeneo ya Mapambano njia ya nyuma kama unaenda Mwenge kwenye miti mirefu bar moja inaitwa kwa jimmy . Kuna vijana 2 walikuwa wanatembea njiani mmoja kabeba begi lake la vitabu ghafla gari ndogo ikampitia kwa pembeni mtu aliyekwepo ndani ya gari akakwapua begi la yule kijana ambapo kulikuwa na simu na karatasi zake . Huyo kijana alipiga kelele kidogo nilikuwa mbele yao nikajua labda ni tatizo lengine kumbe wenyewe wameibiwa bei lao kwahiyo ile saloon car nyeupe ikakimbia moja kwa moja Kijana aliyeibiwa anaitwa Erick Thomas Jongela simu yake anasema ilikuwa na line 2 moja ni 0715 241204 na 0756 816 770 hizi line zilikuwa kwenye simu hiyo iliyokwepo kwenye begi lililoibiwa Mwenzake mwenye simu anaitwa Fadhili no yake ni 0713 76 59 05 Kwa mtindo huu jamani muwe makini mnavyotembea na mabegi yenu pamoja na mali zingine zisivutie sana wahalifu hawa . Nimetoa kisa Hichi kama tukio la kweli lililomkuta mtu naamini tigo pamoja na voda kwa kushirikiana na vyombo vya dola vitaweza kufuatilia simu ya kijana huyo na kuweza kupata taarifa zingine zinazohusiana na simu hiyo toka ilipozimwa mara ya mwisho. Habari kwa mujibu wa blogu ya Othman Michuzi CommentsMama D 14/03/2010 10:32pm
Ni kweli. Tukio kama hilo liliwahi mpata rafiki yangu maeneo ya Masaki hawakufanikiwa kulichukua kwa kua alilishika kwa makini wakamwangusha tu chini na kumburuza kwenye vumbi pembeni ya barabara na waliposhindwa wakakibia.Hao wezi wanalenga hayo mabegi wakijua ni computer. kwa hiyo hasa wabeba computer wawe makini wanapotembea barabarani.
Reply
Salma 14/03/2010 11:12pm
Hili ni tukio la kweli. Maeneo ya Masaki imekua kama kitu cha kawaida. kuna wafanyakazi wenzetu wawili waliibiwa kwa mtindo huo. mmoja aliibiwa laptop na mwingine hand bag yake.
Reply
14/03/2010 11:27pm
Mama D na Salma,
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed