![]() Timu ya Yanga (Obren amevalia fulana ya njano, kaptula nyeusi na soksi nyeupe) Mlinda mlango wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga, bwana Obren Circovic ameshaichezea Yanga kwa takriban miaka miwili sasa. Katika mazungumzo yake na kitengo cha michezo cha shirika la utangazaji habari la Uingereza (BBC Sports), kipa huyo mwenye asili ya Serbia anakubali kuwa vipo vitendo vya kishirikina katika soka ya Tanzania. Kwa mara kadhaa sasa tumekuwa tukisikia habari za hapa na pale kuhusiana na matumizi ya 'ndumba' na vitendo vya uchawi pamoja na ushirikina. Tumeyasikia haya katika nyumba za ibada mf. kanisa la TAG Mikocheni, pia tumesikia yanayotokea kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, yaani albino, tumesikia pia kilichotokea katika hospitali ya Taifa Muhimbili pale kijana alipokutwa na kichwa cha mtoto mdogo na kuelezea mazingira alikokipatia na alikokuwa akielekea, tumesikia vile vile katika Bunge la Jamhuri ya Muungano pale baadhi ya watu walipokutwa wakinyunyiza unga fulani kwenye viti vya wabunge, tusisahau kile cha walokole vs mganga kilichotokea Tabata na hivi majuzi tumesikia tena kile kisa cha mfanyakazi wa ndani aliyerejeshwa kwao Morogoro na wiki iliyofuatia tukasikia habari za 'kutunga' za kisa cha mtu kutoa msaada kisha mikono kuota mnyoya, na visa kadha wa kadha ambavyo havijagonga vichwa vya habari lakini vinasimuliwa mitaani. Jambo hili angalabu si jipya katika nyanja za michezo kwani mara nyingi sana tumesikia habari za wachezaji wa timu kubwa kubwa na maarufu kama Simba au Yanga wakihusishwa na matumizi ya 'ndumba' katika kutaka kupata ushindi hasa pale wanapokutana. Mara timu imetia kambi Bagamoyo kwa 'mafunzo maalumu' au kwenda Zanzibara kwa ajili ya 'kujiandaa' kupambana na watani wao. Akizungumza na BBC, pamoja na mazuri mengi ya kusikia soka la Tanzania hasa akilinganisha na lile la Serbia, kipa Obren anasema, "That witchcraft wasn't mine, it was for some of the other players from Tanzania,"... "I have heard of that [witchcraft] but I don't believe in it, I've had contact with it, but I don't believe in that." Anaongeza kusema kuwa, amejitahidi kuzungumza na wachezaji hao kuhusiana na 'ndumba' lakini wao humsikiliza, wakaitika kwa midomo yao lakini vitendo vyao haviendani na kauli zao, "I've spoken to them but all of them are saying one thing and doing another,"... "They say 'we don't believe in that' but tomorrow I see them putting some bottles or something like that [in my goal]." Angalizo aliloliona Obren kwa soka la Tanzania na maoni yake ikiwa tunataka kufikia kiwango cha Ulaya ni kuwa, "The problem here is behaviour, behaviour here are not at a high level; they must change how they play on the pitch, how they play in training,"... "Behaviour, lifestyle they must change, because your performance depends on behaviour, you must improve yourself." Kwa habari kamili, bofya linki ifuatayo: news.bbc.co.uk/sport2/hi/football/africa/8534075.stm CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed