Tujifunze Kiswahili sanifu. (1) Tunasema “Mahakama hii” (2) Tunasema “Mamlaka haya” (Uwezo/madaraka) “mamlaka hii” (chombo/asasi) (3) Tunasema “Wakala huyu” (mtu anayefanya kazi ya uwakala) “wakala hii” (chombo/asasi inayofanya kazi ya uwakala) (4) Tunasema “Wawakilishi” (watu wanaowakilisha) “wawasilishaji” (watu wanaowasilisha) (5) Neno “Maombi” lina umoja na wingi: “Ombi” (umoja) “Maombi” (wingi) (6) Neno “Saa” halina wingi. “Masaa” si matumizi sanifu. (7) Neno “Wimbo” ni sanifu. “Mwimbo” si sanifu. Imeandikwa na: R. Njau Mdau na mtetezi wa Lugha ya Kiswahili. Dar Es Salaam, Tanzania. CommentsAlex 24/03/2010 6:39pm
R. Njau, Asante sana kwa utetezi wa Lugha ya Kiswahili. Endelea na kazi nzuri.
Reply
25/03/2010 12:57am
Asante sana Bw.Alex kwa kuungana nami katika utetezi wa lugha ya Kiswahili.Inasikitisha sana kuwaona wadau wa lugha ya Kiswahili wakiendelea kuwekeza rasilimali zao katika maendeleo ya lugha za kigeni.Lakini wanasahu kuwa muacha asili ni hasidi na jasiri haachi asili.
Reply
Paul.misalaba 25/03/2010 3:49am
Enyi Alex na Ephraim Kwanza ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kuwa waswahili kiasi hicho. na asante kwa kuw watetezi wa Lugha yetu ya Taifa .Lakini hamjitokezi katika michakato mkapeleka pendekezo katika wizara /Idara /Baraza la kiwsahili la Taifa mkakaosoa maana kiswahili tangu enzi za ukoloni kilihalibiwa na wazungu baada ya kufanya usanifishaji wao mwaka 1959 ,badala yake wakaongeza msamiati wa kigeni Mfano ''shirt;---shati. Sherlar ; shela; kijerumani ,Kwahiyo utaona sisi huwa tunafuata matamushi yaleyale ya wenzetu.Lakini watetezi walio hai kama wanazuoni hawa walipo sikia neno feni ---Fan---walikaa wakajadirijuu ya chombo hicho wakakiita ;Kiyoyozi,mwaka1989 ,Haooo akina Senkolo na nkwera.Hao ndo wako hai .Sio kwamba nawaponda hapana ninatoa Changamoto. badal yake sisi wenyewe tunapo ingia mitaani tunaanza kuharibu ,mara eee mbona unamiminika eti mbona unakonda.hakuna kusifiana kwenye hamna ,HOME WORK
Reply
veronika 25/03/2010 4:25am
neno sahihi ni jamhuri ya muungano wa Tanzania,mimi ndo naona hivyo kwa uelewa wangu.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed