wavuti
wavuti logo Facebook icon Facebook icon Twitter icon Subscribe RSS
 
Pengine utaniuliza, 'oyaa, unazungumzia nini? Hiyo 'misukule' microsoft inayofunga ndo kitu gani tena?'
N'takujibu hivi, 'misukule' hii kitaalamu inaitwa 'botnet' na jina hili limetokana na muunganiko wa maneno mawili ya kiingereza, "robot" na "network".

Utasema tena, 'kwa hiyo?, mbona bado sikuelewi?'
Sasa sikiza...
Ikiwa una anwani pepe, huenda hutakuwa mgeni wa barua mazagazaga (spam na junk mails) yanazokuja kwenye inbox yako bila wewe kujua yametoka wapi na hao waliotuma mbona huwafahamu na isitoshe, wamejuaje anwani yako? Mara nyingi emails hizi huwa zinachujwa na kufichwa kwenye 'junk' au 'spam' folder' na kisha kutupwa ikiwa hutazishughulikia ndani ya siku kadhaa.

Sasa kuhusu uhusiano wa botnet na tarakilishi (computer) na mazagazaga (junk/spam) uko hivi.
Baadhi ya tarakilishi zinaweza kugeuzwa kuwa 'msukule' au 'zezeta' na hivyo kufanyishwa kazi kinyemela (remotely) na mtu aliyeko mahali fulani popote duniani. Tarakilishi inaweza kugeuzwa msukule ikiwa utapakua virusi kutoka kwenye barua pepe au tovuti fulani ulizotembelea na kupakua virusi kwa kutokujua. Punde virusi huyo anapoingia kwenye tarakilishi yako, si rahisi ufahamu kwani huwa haifanyi lolote zaidi tu ya kujishikiza kama kupe na kutoa taarifa kwa yule aliyeko kwenye 'control room' na kusubiri tu kupewa amri ya kuanza kusambaza virusi/trojan/linki za matangazo feki ya dawa za viagra nk. Punde tarakilisho yako inapoanza kufanya kazi hiyo, ndipo inapoitwa 'zezeta' aka msukule alias 'botnet'.

Ukitaka kuelewa kwa njia ya picha, tafadhali bofya picha ifuatayo na kuikuza ili kusoma.
Picture
bofya picha kuikuza ili kuona mfano wa nadharia ya utengenezaji na utendaji kazi wa misukule
Sasa iweje watu wanaotumia bidhaa za Microsoft wafurahie?
Ni kwamba, kutakuwepo na punguzo la junk emails zinazozalishwa kuniani kwa siku kwani kampuni ya Microsoft imepewa ruhusa ya muda kutoka kwenye mahakama moja ya Marekani katika jimbo la Virginia Mashariki inayoipa ruhusa Kampuni hiyo kubwa kabisa ya tarakilishi, kuweza kufungia majina ya intaneti yapatayo 277 ambayo yamethibitika kuwa kitovu cha msukule wa Waledac. Msukule huo unaaminika kusambaza virusi bilioni moja (1,000,000,000) kwa siku moja tu duniani kote. Bofya picha yenye ramani hapo chini ili kujionea makaridio ya tarakilishi ambazo zimeshambuliwa na 'misukule' kote duniani. Kwa maelezo zaidi kuhusu habari hii, soma tovuti ya Microsoft.

Vile vile unaweza kubofya hapa ili kutizama video kusikia maelezo mafupi kuhusiana na suala hili.
Picture
bofya picha kutizama athari ya virusi wanaosambazwa na misukule ya tarakilishi
 


Comments


Comments are closed.