Balozi mdogo wa Japani nchini Tanzania ambaye pia ni mtaalamu wa maswala ya uchumi, Yoshiyasu Mizuno ametembelea mvumbuzi wa jenereta la kutumia hewa kufua umeme. Katika picha zifuatazo, balozi huyo anaonekana akiwa na mvumbuzi mwenyewe pamoja na wataalamu wengine kutoka Tanzania Industrial Research Development (TIRDO) eneo la Msasani ambapo ndipo lilipo jenereta hilo. Picha kwa hisani ya blogu ya John Bukuku ya Full Shangwe. Commentsfredrick 13/03/2010 12:28pm
Hongera nyingi kwa wataalamu hawa nahisi ni kama baada ya migogoro ya umeme wa tanesco na bei zao kuwa juu ya hali ya maisha ya mtanzania Mungu anatuongoza jinsi ya kujikomboa!
Reply
CONF 13/03/2010 12:44pm
maandishi madogo sana, sijui mlikuwa mna lenga kwa watu gani.Kwanza ni katika italic na madogo sana.sidhani kama mlengwe amefikiwa kwa ufasaha.
Reply
Pastor Kumbuka 13/03/2010 1:52pm
Safi sana kijana,Mungu ametupa akili tuitumie.Endelea Hivyo hivyo iko siku utafanikiwa. Mtaalamu wa kwanza kuvumbua ndege Mjerumani aliitwa Otto Lilienthal- 1891. Alianza kufikiri kwanini PULIZO linaweza kuelea angani, baadaye akaanza kuliongeza mabawa na kufikiri namna litakavyotua popote atakapotaka. Leo hii zinaruka ndege kubwa mno; KLM, LUFTHANSA, BRITISH AIRLINE. Rumi haikujengwa siku moja.Ubarikiwe
Reply
mashaka 13/03/2010 5:10pm
unpoamua kutoa huduma fulani kwa jamii hata pasipo malipo ya aina yoyote hakikisha maamuzi yako pia yazingatie jamii husika,sasa unapofanya mabadiliko fulani jaribu kushirikisha jamii nadhani mabadiliko uliyofanya kwa aina ya maandishi utumiayo sasa ni ya kujifurahisha wewe binafsi labda na kundi fulani la wasomaji wako .mimi niko nje ya nchi nimsomaji wako mzuri sana lakini hii haikunifurahisha.
Reply
Mashaka (et al),
Reply
Yonga 13/03/2010 7:14pm
Mpendwa dada Subi, wewe piga mzigo, walau hata wanaolalamika umewapatia nafasi ya kulalamika bila kwanza kufanya juhudi za kutatua tatizo lao. Asante kwa kazi nzuri.
Reply
Mashaka 14/03/2010 1:17am
Nashukuru dada subi kwa marekibisho na ushauri wa kiufundi pia,nakupongeza kwa kazi yako hii nzuri, binafsi nimtembeleaji mzuri wa wavuti naitumaini kujua nini kinaendelea nyumbani kihabari hivyo lalamika yangu ni ya nia njema kabisa juu ya wavuti,jpili nakutakia afya njema na kazi njema.
Reply
Shukran mdau Mashaka.
Reply
14/03/2010 3:21am
Kwanza nampongeza sana huyu mvumbuzi,na hii inaonyesha kama tukihitaji tunaweza sana ila tatizo linalotusumbua ni uzembe wa watanzania wengi(samahani kama nitakuwa nimetumia lugha mbaya)kuona kwamba kila kitu basi ni cha wazungu tu.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |







RSS Feed