Mtoto wa umri wa miezi mitatu wa Bwana Kim Yoo-chul, 41, na mkewe Choi Mi-sun, 25, wa nchini Korea amefariki dunia baada ya wazazi wake hao kumwacha bila huduma yoyote kwa mwendo wa saa 12 mfululizo. ![]() random photo from the internet, not related to this story Polisi wamesema kuwa wazazi hao walikuwa wakilea mwanasesere waliyempa jina la Anima kwenye programu ya Prius inayoendeshwa na 'Second-Life' kupitia kwenye tarakilishi (computer) iliyounganishwa na intaneti katika mgahawa mmoja nchini humo. Mchezo huo humpa mtu ruhusa ya kuwa na ndoto za Ali Nacha kuhusu kazi aipendayo, marafiki anaowapendelea na hatimaye hupewa zawadi za watoto kwa kushinda hatua moja ya mchezo kuelekea nyingine. Wazazi hao waliporejea nyumbani siku moja baada ya kushinda kwa saa 12 mfululizo wakicheza mchezo huo, walikuta mtoto wao wa kweli, ambaye hakuwa na jina, amekwisha fariki na ndipo walipowapigia simu polisi ili kutoa taarifa hiyo. Uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa mtoto huyo alifariki kwa utapiamlo baada ya kukosa chakula kwa muda mrefu. Inasemekana kuwa wazazi hao walikata tamaa ya maisha kwa kuwa hawakuwa na kazi huku wakiwajaaliwa(?) kuwa na mtoto njiti (mtoto aliyezaliwa kabla ya miezi tisa - a premature baby). Hivyo ili kupambana na hali halisi ya maisha iliyokuwa ikiwakabili, ndipo walipoamua kuucheza mchezo huo wa kulea mwanasesere hali iliyochangia kumsahau mtoto wa kweli aliyekumbwa na mauti. YATOKANAYO Ulevi wa matumizi ya tarakilishi na simu zilizounganishwa na intaneti unazidi kukua na kuathiri watu wa rika zote, hasa hasa vijana na watu wa umri wa makamo. Nimewahi kusikia visa vya wazazi kusemana na kulumbana juu ya mmoja wao kutumia muda mwingi kwenye simu (Blackberry, iPhone nk) katika nyakati nyeti kama vile wakati wa kula chakula, ambapo mtu anashindwa kushiriki chakula cha pamoja ama akishiriki basi muda mwingi anautumia kwenye simu badala ya kuzungumza na walioko mezani, wengine wanatumia muda mwingi msalani (uani, chooni) si kwa kuwa wanakwenda haja kubwa bali kwa kuwa wapo 'bize' na simu. Wapo watu waliosababisha au kupatwa na ajali kutokana na matumizi ya simu zenye intaneti. Wengi wao wanapenda kusoma matukio ya papo kwa papo kwenye mitandao jamii kama vile Facebook au Twitter. Hii ni changamoto kwetu sote kuwa makini na muda tunaoutenga katika kutumia intaneti ikiwa ni pamoja na kuwa makini na tovuti ama michezo tunayoipendelea. Ni vyema yeyote anayejiona kuwa muda wake mwingi unamegwa na intaneti, basi ajitahidi kujiwekea ukomo na kutafuta kitu mbadala cha kufanya ili kuondoa utegemezi uliopindukia wa intaneti. Nadhani punde tutaanza kuwapata wasomi na wataalamu spesheli katika nyanja za matumizi ya intaneti na namna ya kupambana na ulevi wa matumizi ya intaneti. Tukifikia hapo, hata mmiliki wa tovuti hii, Subi, anahitaji kwenda 'internet rehab' - si utani. CommentsJide nilihamisha maoni yako toka kule ulikoandika kwenye posti nyingine na kuyaweka kwenye posti husika.
Reply
Hao wakorea waache kusingizia mambo ya internet, walifanya kusudi ili kafe na wao wapunguze tatizo la watu 3 kutokuwa na kazi ilhali wanafakamia misosi. Hata wakilia ni machozi ya mamba tuuuuu.
Reply
ha ha haha LOL ha ha ha hahaa, we Chib, wewe ndiye ligonjwa kabisa kabisa yaani ingekuwa pale kijijini kwetu paleee nyuma ya Makuti mbele ya Peds tungekuweka kwenye kundi linaloangukia kwenye definition ya 'pt NOT aware of their illnesses' wakati siye wengine tungeangukia kwenye kundi la 'pt aware of their illnesses'... sasa wewe ndo unahitaji matibabu haraka sana, yaani ile kengele inagongwa tu, unatakiwa uwe umeshika nambari moja au mbili hivi, nhi hi hii.
Reply
Ha haa haa, si unaona, umeshajibu, yaani computer ipo ndani ya kichwa ha haaa
Reply
Subi, wewe umeamini kuwa mtoto wao amekufa kwa njaa? maana hao wakorea wana tabia ya kuwekea watoto wao chakula mpaka hata toilet ili iwe handy when they are in need. Utanisamehe maan kiswahili kinaanza kunipiga chenga. Takriban miaka 30 sasa toka niondoke Tanzania and kuishi uarabuni
Reply
Ali Diku Mussa 16/03/2010 5:29am
i say sister Subi if there is any solution for those who spends all time for chatting and other thing in internet, i need it cause sina hobby nyengine yoyote zaidi yakubrowse kwenye mtandao. this is me Ali from Nungwi Zanzibar email me : ally.diku@yahoo.com or allydiku@hotmail.com
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed