![]() mmoja wa walioathirika baada ya kutumia maji yaliyotiririka toka migodi Picha zinazoonekana hapa ni mali ya blogu ya Kijijini Kwetu ya Chacha o'Wambura (Ng'wanambiti) na zimewekwa hapa ili kusambaza habari hii kwa watu kwa matumaini kuwa yupo mwenye roho ya ubinadamu walao mmoja atakayesikia na mwenye uwezo wa kufanya jambo la haki au kufikisha suala hili kwa anayeweza kulishughulikia. Masuala kama haya yatatufababisha siku moja tudaiane haki na amani kwa ncha ya upanga, na hiyo si kauli yangu binafsi bali nukuu ya wenye hekima waliotutangulia, mwenye akili na afahamu. Ng'wanambiti anasema: Cha kushangaza ni kuwa kuchukuwa hatua kwa swala hili kumekuwa kukichukua muda mrefu sana. Tunachosikia ni majibu ambayo ni ya kiutawala ambayo Barrick, DC wa Tarime, RC Mara, NEMC, Wizara ya Mazingira, Wizara ya Afya na Wizara ya Madini wanayatoa ni sawa kuwa 'wenyeji wameiba lining za mabwawa ya kuhifadhia maji machafu'. Je na hawa ambao wako katika vijiji vilivyo mbali na mgodi ambao ndo wamedhurika kwa kiasi kikubwa ni wezi? Ndo kusema kuwa wataalamu wetu wa afya kuanzia Mkemia Mkuu wamewaasi wananchi walowasomesha kwa jasho la kodi zao na kuungana na wawekezaji kwa kisingizio cha 'attracting foreign direct investment? FDI kwa gharama za wananchi wetu? Je kuna mkono wa mtu (kisiasa na kampuni)ama ni kutojali kwa viongozi wetu? CommentsBahati 08/03/2010 4:10pm
Hizi picha ni aibu kwa nchi kama Tanzania, umasikini wetu, utajiri wa madini runaona. Hivi inakuwaje sisi tunakuwa watumwa wa wageni kwenye nchi yetu wenyewe?. Nafiri WIzara ya Nishati na madini inawajibika. Na Wizara ya afya inafuatia kwa kutoa huduma tu, Wabunge walione hilo sio kutaka kura bila kuangalia wateso ya wananchi.
Reply
alledros 09/03/2010 7:23am
Sawa Bahati! TZ inatawaliwa na wageni wengi na aina nyingi, lakini!!!!
Reply
alfred 09/03/2010 10:16pm
watanzania lazima tuangalie viongozi tunaowachagua,maana viongozi wa sasa uzalendo hakuna.ni lazima tuchague viongozi watakaokubali kufa kwa ajili ya wananchi wao na siyo wanaotuuza na kutufanya watumwa ktk nchi yetu wenyewe. KILA ALIYEHUSIKA KATIKA MIKATABA HII YA MADINI AMBAYO IMELETA MADHARA KWA WATANZANIA WENZETU ATASIMAMA MBELE YA HAKI SIKU HIYO IKIFIKA NA ATAHUKUMIWA KAMA ALIVYOHUKUMU WATANZANIA WENZAKE,ATASALITIWA KAMA ALIVYOWASALITI WATANZANIA WENZAKE.
Reply
john 10/03/2010 4:53am
Who don care so far the victim is not a top leader in the govt.
Reply
Paul. 11/03/2010 6:04am
Jamaniii inasikitisha sana tunaposhindwa Hata sisi wenyewe ati mpaka viongozi ,maana tunajua kuawa viongozi wetu hata msimamo hawana .Ninaomba kila anaeye mtanzania ashiriki kikamilifu katika kusaidia wenzake Sawa Jamani ,La' sivyo makaburu watatumariza.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |











RSS Feed