Simba 3 JKT 1 06/03/2010
Ilikuwa ni dakika mbili za mwisho za kipindi cha pili zilizoipa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania, Simba SC ushindi wa magoli 3 - 1 dhidi ya timu ya JKT Ruvu. Simba inahitaji pointi mbili tu ili iweze kutangaza ubingwa wa kabumbu Tanzania Bara katika msimu wa Vodavom Premier League 2010/2011. Ikiwa Simba itafanikisha hilo, hii itakuwa historia mpya kwani tangu kuanza kwa ligi hiyo, Simba haijawahi kupoteza mchezo hata mmoja isipokuwa kutoshana nguvu katika michezo miwili tu ilipocheza na timu ya Kagera Sugar ya na African Lyon. Magoli ya Simba yalifungwa na Mussa Hassan Mgosi 2 (moja kila kipindi) na Uhuru Selemani. Goli la JTK Ruvu lilipatikana kipindi cha kwanza kwa njia ya penati. Photo credit: PwaniRaha.com, IssaMichuzi blog na Full Shangwe blog. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |














RSS Feed