Ni swali alilouliza Paul Misalaba siku chache zilizopita kwenye kisanduku cha maoni na bado halijapata jibu.

Swali: Tusaidianeni katika kunyosha utata huu katika sentensi ifuatayo JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA na JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA.
Ipi ni sentensi sahihi kati ya hizo sentensi mbili?

Paul
 


Comments

mashaka
31/03/2010 04:46

Sahihi tunasema muungano huu ni wa aina gani na si ya aina gani ni wa kimajimbo au nchi mbili huru ,kwahiyo sahihi ni jamhuri ya muungano wa tanzania.mf ndoa ni muungano wa watu wawili. ya inaonyesha umiliki wa jamhuri ya muungano ninani?na haionyeshi ninani walioungana.

Reply
David Fred
31/03/2010 09:41

Halo bwana Paulo. Kuna tofauti ya matumizi ya neno /kiunganishi 'ya' na neno/kiunganishi 'wa'.Neno 'wa' linaonesha muunganiko wa vitu viwili na wakati mwingine hata umiliki wa kitu.mf. umoja wa wanafunzi,kuku wa Abdala .Neno 'ya' linatumika kuelezea kitu(kuelezea maana ya kitu)mf.Siku ya uhuru(hii inaelezea hiyo siku ni siku maalumu ya kuadhimisha uhuru) .
Kwa kwa jina la Tanzania kama nchi huru inayoundwa na Muungano wa nchi mbili tunatumia kiunganishi/neno 'wa' kuonesha kuwa huu muungano unamilikiwa na Tanzania(United Republic of Tanzania).Neno sahihi ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Reply
Subi KNY Monsignor (comment via GBuzz)
31/03/2010 11:49

Inaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania..rejea Katiba ya mwaka 1977 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2000. Soma kichwa cha habari cha katiba yenyewe pia anza kuingia ndani uk 9 tunapotangaza jina la Tanzania kwenye sheria ya 1984 Na.15 ibara ndogo ya 3utaikuta......Mazoea yana tabu, sijui kwa sababu ya urahisi wa kutamka ya badala ya wa..

Reply
31/03/2010 14:11

“YA” inarudi kwa Jamhuri wakati “WA” inarudi kwa muungano. Kwa hiyo usahihi ni jamhuri ya muungano WA Tanzania. Hapa tunasisitizia muungano na siyo Jamhuri.

Reply
Paul
31/03/2010 21:51

Nashukru sana kwa michango yenu mizuri juu ya hili swali.
Lakini inasikitisha tunapoona waandishi maarufu kama akina Nyambari Nyangwine iwapo wanapotosha kwa kuandika -YA-Badala ya -WA- kwenye vitabu vingine vya A-Level .kweli siyo vizuri.Maana maelfu ya wahitimu wanaomaliza ama kuhitimu hivikaribuni wote wamerishwa sumu hiyo.
Asante
Paul.

Reply
Mbwambo
11/04/2010 09:00

Hii iko wazi. Sentensi sahihi ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ukitumia "ya" badala ya "Wa" lazima usitaje neno "Jamhuri" ila utaje neno kama "Nchi".

Reply



Leave a Reply