Ripoti tuliyoipata inasema kuwa basi la kampuni ya Shabiby lililokuwa likitoka Dar Es Salaam kuelekea Dodoma limepata ajali mbaya sana eneo la Ubena baada ya kugonga nyuma ya lori. Taarifa inasema kuwa miili ya watu imetapakaa barabarani. REKEBISHO Kwa mujibu wa blogu ya Maggid Mjengwa, ajali ni ya basi la Shabiby lilolokuwa likitokea Arusha kwenda Dodoma. Ajali ilitokea majira ya saa kumi. Mabasi ya Shabiby na Mohamed Trans inasimuliwa na abiria kuwa yaliendeshwa katika mwendo wa 'mashindano'. Kwenye msitu wa Mwidu ikatokea hali iliyosababisha dereva wa basi la Shabiby kushindwa kumalizia ovateki na hivyo kulivaa lori. Picha zinazoonekana (bofya kuzikuza) ni kwa hisani ya blogu ya Mjengwa; ziada tafadhali bofya hapa. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |










RSS Feed