
Tunaomba wasomaji na wapenzi wa wavuti.com wafahamu kuwa hatujarekebisha ukurasa huo zaidi tu ya 'update' zinazofanyika kila tunapokuwa na taarifa mpya, jambo tunalolifanya tangu awali.
Tumejaribu kutafuta chanzo cha tatizo ili kujua kama ni upande wetu, code za pleya, ama host wetu na kugundua kuwa hizo zote zipo vyema kabisa.

Hivyo basi tumehitimisha kuwa tatizo lipo katika settings za Windows Microsot kwenye browser yao ya IE bila kujali toleo.
Tunawashauri watu wote wanaotaka kusikiliza audios wapakue na kutumia mojawapo ya virambaza tulivyotaja hapo juu kuwa vinafanya kazi vyema. Virambaza hivi hupatikana bure.
Unaweza kujiipakulia kwa kubofya jina la kirambaza; itakupeleka katika tovuti ya kirambaza husika. Ukikwama katika kupakua ama kuchomeka kwenye tarakilishi unayotumia, tafadhali wasiliana na mhusika wa kitengo cha IT wa eneo uliloko.
Sisi wahusika wa wavuti.com hatutaingia tena gharama yoyote ya kutafuta na kubadili pleya ili ionekane katika IE kwani huduma hiyo inapatikana bure kwenye virambaza vingine. Tumefanya lililo ndani ya uwezo wetu, tafadhali nawe (nanyi) mfanye yaliyo ndani ya uwezo wenu; ikishindikana, basi tusameheane.
Asanteni na poleni kwa usumbufu.


RSS Feed