Habari ya Kazi, Mimi ni mdau mkuu wa blog wako, kuna shida ambayo huwa inanitatiza sijui kama ni mi peke yangu au hata baadhi wateja yamewakuta haya. Mwaka jana Benki ya Exim imetambulisha huduma mpya au akaunti mpya inaitwa FAIDA akaunti kutokana na matangazo yao wanaonyesha kwamba ukipata hiyo kadi kuna faida nyingi ikiwemo ku nunua bidhaa kwenye mtandao (on-line purchasing), haya matangazo yamenishawishi kufungua akauti ya FAIDA, sasa mpaka leo hii asubuhi hii najaribu kuweka details ya hiyo Faida Card ambayo ni Debit Master Card naambiwa kuwa ajili kwa kununua bidhaa "You have entered an invalid number or partial credit card or debit card number. Please check your entry and try again", Tafadhali naomba wahusika wa Exim bank watupe statement yao kuhusu hilo suala, kwa sababu wametufanya tuhamishe fedha kutoka kwenye benki nyingine na kuweka kwenye hiyo account tukitaraji kwamba tuta purchase on-line kumbe hamna kitu, sasa huu sio uongo wa ki macho macho na kupoteza uaminifu wenu kwenye jamii ya Watanzania? Nawasilisha Meza kuu... Wake Mteja wa Faida na Mdau wa Blog CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed