![]() bofya picha kuikuza Kadiri siku zinavyosonga, ndivyo na watu wanavyotumia intaneti na kadiri ya matumizi ya intaneti yanavyoongezeka ndivyo na vitendo vya kidanganyifu na wizi wa mitandaoni vinavyoongezeka. Kujifunza kung'amua mbinu wanazozitumia matapeli katika kufanikisha malengo yao ndicho kiokozi muhimu katika kujilinda wewe binafsi na wale unaowajali dhidi ya upotevu wa fedha na mali. Kwa bahati mbaya, matapeli kama ilivyo kawaida yao, hawakomi kujaribu kuvumbua mbinu mpya za kuiba pale wanapogundua kuwa watu wengi wameshazifahamu na kuzizoea mbinu zao. Siku tatu zilizopita nimepokea ujumbe kama unavyosomeka kwenye picha inayoonekana hapo (bofya kuikuza ili kupata ukubwa unaosomeka kirahisi zaidi) na katika ujumbe huo, hakukuwa na maelezo zaidi ya 'respond to the subject matter'. Nilifungua kiambatanisho hicho na kusoma maelezo hayo. Yafuatayo ni mambo muhimu ya haraka niliyotumia kung'amua kuwa ujumbe huu ni wa kitapeli.
TAHADHARI: Tafadhali usiige tabia ya kufungua viambatanisho vyovyote navyotumiwa ikiwa huna usalama wa anti-virus katika kompyuta unayoitumia. Baadhi ya watu hufungua viambatanisho wasivyotarajia kupokea kwa kuwa wana tamaa ya kujua kilichomo ndani. Matokeo yake ni kufungulia virusi wanaoharibu tarakilishi taratibu au kuisababisha iwe 'misukule' (zombie) kwa ajili ya kutumika kutuma virusi kenye tarakilishi nyingine bila ya wao kufahamu. Mara nyingi viambatanisho (attachments) huwa ni vyanzo vya kusambaza virusi kwenye tarakilishi. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed