Habari hii imeandikwa katika gazeti tando la HabariLeo

Mmomonyoko wa maadili unaelekea kuiathiri jamii ambapo sasa baadhi ya viongozi wa dini wanazidi kuingia matatani kutokana na kushiriki katika vitendo vya ngono.

Mchungaji wa kanisa la African Inland - (AIC) ambaye pia ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Chona, wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Pasia Dickson (36), ametuhumiwa kufumaniwa Jumatano akifanya mapenzi na mwanafunzi wa darasa la saba.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Daudi Siasi amethibitisha tukio hilo akisema kwamba, mtuhumiwa ameshatiwa mbaroni na amefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kubaka na kushambulia.

Siku ya tukio mwalimu huyo alikwenda nyumbani kwa mwanafunzi huyo na kufanya naye tendo la ndoa chumbani kwa mama wa mwanafunzi, ambaye wakati wa tukio hilo alikuwa amekwenda gulioni kununua mahitaji ya nyumbani.

Naye Diwani wa Kata ya Chona iliyopo umbali wa kilomita zaidi ya 50 kutoka Kahama Mjini, Mabala Mlolwa amesimulia tukio akisema kwamba, alishiriki kwa kiasi kikubwa katika kuyaokoa maisha ya mchungaji huyo.

Ni tukio la kweli, na mimi nimeshiriki katika kumnusuru kwa sababu baada ya fumanizi alijiokoa kwa kumng’ata kaka wa binti na baadaye alitimua mbio akiwa mtupu hadi kwenye ghala la kuhifadhia nafaka katika nyumba ya jirani. “Wananchi wenye hasira walitaka kummaliza huko huko ghalani, nikawasihi wasubiri polisi na kweli baadaye polisi walikuja kumchukua, mimi ndiye niliyemchukulia nguo, na sasa wanamshikilia …”

Mashuhuda wa tukio hilo wanaeleza kwamba, Mchungaji huyo alikuwa na uhusiano wa muda mrefu na mwanafunzi huyo. “Hata siku ya tukio, jamaa alikwenda akijua kabisa ratiba ya mama wa mwanafunzi, bila woga alikwenda na pikipiki akaiegesha nje naye kuzama ndani na hawara yake…  Kaka mtu ndiye aliyeshitukia mchezo mchafu wa mchungaji, kwani alipofika nyumbani alishangaa kuona pikipiki nje, baada ya kuingia ndani alimkuta mchungaji huyo katika kitanda cha mama yao akiwa utupu wakifanya mapenzi na mdogo wake mwenye umri wa miaka 16... ndipo katika kukurupushana huku mchungaji akitaka kutoka akiwa utupu na kaka mtu akijitahidi kumzuia kutoka huku akipiga kelele, mchungaji aliamua kumng’ata kaka mtu na kukimbia, lakini hakufika mbali kwa sababu hakuwa na nguo,” alisema Mlolwa.

Kesi ya Mchungaji Dickson inatarajiwa kuendelea Aprili 30, mwaka huu.

MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI
Pumbaf kabisa!
 


Comments

Mtoto wa mkulima
18/04/2010 14:48


Da Subi yaani hawa, hela ya EPA, RICHMOND, KILIMO KWANZA na nyinginezo hazijawatosha? Jamani..watu hawana hata aibu..anyway..waliokula watachangia kusudi waendelee kula.

Duh..Tanzania yetu hii..yataka moyo!

Reply
Paul.
19/04/2010 04:08

Kweli Dada subi nimepatwa na msituko wa ajabu nilipo sikia mchungaji kafumaniwa ,ikabidi nifuatilie nikamuuliza Babu mchunaji Aic mwanza makongoro kuhusiana na tukio hilo ambalo limetikisa hata wakristo wa makanisa mengine, kulikoni?Babu ,mchungaji Joseph-Gisai na ndo Ktibu mkuu AIC,Tanzania , Nina nukuru alivyosema ''Hata mimi limenisitua pamoja na maasikofu wote ikabidi nifua atilie nikajionee, ''amesema huyo si mchungaji Bali ni muumini wa kanisa hilo na nimwalimu wa shule ya msingi ilyopo hapo,waosema hayoo ni watu wasio na mapenzi mema na kanisa la mungu wanashindwa kusema ukweli ,wanaamua kusema ukweli;; Hata mimi nasema Mwongo ni aadui wa haki na ni Rafiki wa shetani,wasomaji wote mnaopitia mtandao huu tuandikeni habari za ukweli sio kushuhudia uongo inachafua watu na kubandika watu vyeo ambavyo si vya kwao na kutoa maneno ya kuchafua makanisa Hebu tujioneni sisi ni watanzania na ni hekalu la mungu lisilo na taka ,,Wagalatia5;19-21
na tubadilike sio tu kusambaza habari za uongo, toeni changamoto za kufundisha , za kuchekesha,zenye ucheshi ,tunaposema za kufurahisha na sio matusi,tutumieni vyombo ambavyo watu hawa wametoa bure kwa manufaa bora na sio bora manufaa.katika kujenga na kuelimisha watanzania wenyewewe ambao ni sisi,na uliye andika hivi mungu akuone .kwa upande wangu mimi siwezi kushambulia dini ya mwenzangu unless otherwise ang'atuke yeye mwenyewe,Biblia inasema shika sana ulichonacho mwivi asije akakupokonya,
,,,kuweni makini asante

Reply



Leave a Reply