Kwa baadhi ya watu niliahidi kuisoma kumbukumbu hiyo na kuiweka katika sauti kwa ajili ya yeyote ambaye anapendelea kusikiliza sauti (audio) zaidi ya kusoma maandishi.
Vipo vipande viwili vya audio:
- Acapella - yaani kusoma kumbukumbu tangu mwanzo hadi mwisho bila ya kuwepo wimbo wowote.
- Musical - yaani kusoma kukiambatana na sauti ya muziki. Ndani ya audio hii zinasikikika nyimbo tatu. Katika background ni wimbo wa Enya - Adiemus na Wimbo wa Taifa ubeti wa kwanza - Mungu ibariki Afrika na kisha ubeti wa pili unasikika pekee - Mungu ibariki Tanzania, mwishoni ni Ukombozi wa Afrika utunzi wake - Patrick Balisidya.


RSS Feed