Kuna mtu anaweza kunifahamisha umbumbu wangu wa TEKNOHAMA?.
Hivi blogu ya Ikulu ya Tanzania inaendeshajwe? Haina habari za kila siku?Hivi yote yanayotokea Tanzania, ziara za waziri mkuu hivi karibuni, mama Salma Kikwete, Rais Kikwete safari zake zote za mwezi mzima uliopita, risala zake, hotuba zake, angalau hayo tu yanashindikana kuwekwa kila siku?
mawasilianoikulu.blogspot.com
Hivi idara ya mawasiliano ya Ikulu hawalioni hili?
Leo Jumapili 18.04.2010. Habari za mwisho kwenye blogu hiyo ni za Machi 18. Mwezi mzima umepita. Matukio mengi yamepita katika kipindi hicho, lakini hakuna hata picha wala nini. Tunaona picha kwenye blogu ya Michuzi, Mjengwa, Hakingowi, Mrocky, Wavuti na nyinginezo za watu binafsi.
Ikulu ka!
Basi wacha blogu, tovuti ya taifa la Tanzania, ndo´kichekesho! Manaake habari haziko katika mpangalio. Ziko shaghalabaghala! Angalieni wenyewe hapo: www.tanzania.go.tz
Mbona tovuti za wizara mbali mbali habari zake ziko katika mpangilio? Hii ndio sura ya Tanzania nje ya nchi, lakini mwee?sisemi mengi.
Hata tovuti ya Waziri Mkuu www.pmo.go.tz inapendeza iko katika mpangalio mzuri.
Wenu Tausi Usi Ame Makame,
Oslo
(anwani pepe imehifadhiwa)
YATOKANAYO
wavuti.com inaunga mkono kilio cha Tausi na Watanzania wengine ambao tumekuwa tukipiga kelele kila leo, hasa Dk. Faustine ambaye ameandika mara kwa mara kuhusiana na kero hii lakini inaonekana kelele hizi ni sawa na za kupigia mbuzi gitaa. Watanzania tunapenda turinge kuwa nasi tupo katika karne ya Sayansi na Teknolojia katika TEKNOHAMA lakini tunashindwa kujivunia hata kuthubutu kuhadithia ati tuna mkondo wa mawasiliano ya uliofunguliwa rasmi na Raisi mwaka jana na sasa kuna ujio wa EASSy cable.
Tafadhalini wahusika wa IT Serikalini tuondoleeni hili kwani sisi tupo tayari kuitangaza e-Tanzania.


RSS Feed