Ni jambo la kusikitisha sana, kwamba baada ya kukemea, kufikisha washitakiwa mahakamani na hata hukumu kutolewa, pamoja na juhudi zote zinazofanyika katika kupambana na dhuluma hii ya kukata viungo ya miili ya binadamu wenzetu kwa imani potofu tu kutokana na rangi yao ya miili, inaendelea.

Anayeonekana pichani ni mtoto Kabula Nkalango akiwa na dada yake Regina Cosmas baada ya kufanyiwa ukatili wa kukatwa mkono wake wa kuume na watu saiofahamika. Watu hao waliondoka na mkono huo. Ukatili huu ulifanyika katika kijiji cha Luhaga, kata ya Igwamanoni, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Huu ni ushetani na wote wanaofanya hivi na kuamini hivi wanaongozwa na roho wa shetani.

Picha kwa hisani ya Mroki Mroki.
 


Comments




Leave a Reply