![]() kisanduku kilichokuwa na fedha Wanandoa wamoja huo nchini Australia wameshitakiwa kwa kosa la kujipatia fedha kwa kutokuonesha uaminifu. Wanandoa hao walikumbwa na shitaka hilo pale walipokwenda katika duka la kuuza vifaa vya mtumba na kununua kijisanduku ambacho ndani yake kulikuwamo dola za Kiaustralia laki moja (100,000). Fedha hizo zilikuwa zimehifadhiwa kwenye kijisanduku hicho na wazee wawili waishio katika kitongoji cha Beaconsfield huko mjini Melbourne nchini Austalia. Mmoja wa wazee hao, mke, hakufahamu kuwa mumewe amelikificha fedha zao katiak kijisanduku hicho na hivyo yeye kukitoa kwa shirika la Jeshi la Wokovu (Salvation Army) kwa ajili ya kuuza. Mumewe alipogundua kilichotokea, aliharakisha kwenda kwenye duka la Shirika hilo kujaribu kukipata lakini ilikuwa bahari mbaya alichelewa kwani kijisanduku chenyewe kilikuwa kimeshauzwa. Harakati za kukisaka zilifaniiwa kugundua kuwa kijisanduku kilikuwa kimeuziwa wanandoa waliokinunua na kulipia kwa kutumia kadi ya benki. Polisi walikipata kijisanduku lakini walikuta kuwa fedha zilishachukuliwa na kuwekwa kwenye akaunti mpya ya benki. Kiasi fulani cha fedha hizo kimepatikana. Wahusika wameshitakiwa kwa kosa la 'theft by finding'. KISA HIKI KIMENIFUNDISHA NINI? Dhana ya ubinadamu imekuwa kitu adimu sasa. Tusichoke kutenda wema. Tusiache kuwa waaminifu. Tusipende vya bure. CommentsBahati 08/04/2010 5:46pm
Aliyenunua hana kosa, aliuziwa kisanduku na mali iliyomo ndani yake. Mwenye kuuza alitakiwa kujua ndani kuna nini. Ndiyo maana mtu akipewa zawadi ni wajibu wake mpewa kufungua ili kujua kilichomo ndani.
Reply
samuel 14/04/2010 4:40am
Wangewaacha tu wale hela zao , ilikuwa bahati , si unajua bahati inaweza ikakujia .....lakini au wakiwarudishia na wenyewe waonyeshe usamaria(wawakatie kidogo ya kupoza maumivu ).
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed