Ripota wa CloudsFM aliyehojiwa na Gardner Habash na Ephraim Kibonde katika kipindi cha Jahazi, amesikika akisema kuwa boti ilibinuka na kumwaga kila kilichokuwamo na kwamba maiti nane walikuwa wameshapatikana.
Baadaye, Kamanda wa Kikosi cha Polisi mkoani Lindi Steven Buyuya alisikika katika kipindi cha Dira ya BBC akizungumza na Mtangazaji wa habari wa BBC, Josephat Mwanzi, na kuthibitisha kuwa ajali hiyo imetokea hapo Mtwara wakati boti ilipokuwa ikivusha abiria kutoka Shangaji (mwendo wa km. mbili toka Mtwara bandarini) kwenda Msangamkuu, wengi wao wakiwa ni wavuvi na wafanya biasahara ndogo ndogo.
Boti hiyo imesajiliwa kwa uwezo wa kubeba watu kumi na nane (18) lakini walikuwepo abiria kumi zaidi hivyo kufikia idadi ya watu ishirini na wanane pamoja na mizigo na baisikeli za wasafiri.
Inasadikiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kuzidiwa uzito (overloading) na hivyo kukosa stamina.
Mmiliki wa boti hiyo pamoja na baharia wake wamekimbia.
Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa vifaa vya uokozi na kusaidia katika zoezi hilo.
SAHIHISHO
Sahihisho kidogo, nadhani kuna makosa kwenye uwasilishaji wa taarifa hii. Marine Parks ni taasisi ya Serikali (chini ya wizara ya mifugo na uvuvi), na haimiliki boti za kusafirisha abiria, ina boats zake kwa ajili ya surveillance and enforcement in the ''marine park'' boundaries. Na pia kwa maelezo yaliyotolewa hiyo boat imezama toka ''kivukoni landing site'' eneo ambalo liko Mtwara mjini nje kabisa ya mipaka ya ''marine parks''.
Shukrani kwa Eliabu Thomas kwa kutoa rekebisho hili (kama inavyosomeka kwenye sehemu ya maoni).


RSS Feed