Jeshi la polisi Kamanda Dar es salaam kwa kushirikiana na kampuni ya simu za mkononi Tigo wameunda kikosi kazi kwa madhumuni ya kudhibiti wizi wa miundo mbinu kama vile betri za minara ya simu, vipuri vya majenereta na mafuta.
Picture
Suleiman Kova - Kamanda wa Polisi Dar
Kamanda wa Polisi kanda maalum ya polisi Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema wizi wa miundo mbinu wa mara kwa mara sasa umekithiri.

Wezi wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za wizi kwa kujifanya wao ni watumishi wa kampuni hiyo na hatimaye kufanikiwa kuiba.
Wizi huo umegharimu mamilioni ya fedha dhidi ya kampuni ya Tigo hivyo kuathiri mapato ya kampuni ya Tigo na nchi yetu.

Ili kupata ufanisi wa operesheni hiyo, wananchi wameombwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kwa namba 0715 123888, mtu yeyote atakayekuwa na taarifa atume ujumbe, ujumbe utakuwa ni bure hautakuwa na tozo lolote.


Aidha, kampuni ya ulinzi ya Kiwango inayoshughulikia ulinzi wa minara itakuwa inatumia namba 0715 123444 kwa kupitia namba hizo utoaji taarifa utakaombatana na mafanikio utamfanya mtoaji taarifa kufanikiwa kupata donge nono lisilopungua shilingi milioni moja na kuendelea, hii ni kwa kutokana na uzito wa taarifa yenyewe.

Pia wananchi wameonywa kutonunua betri za aina hiyo kwa matumizi yasiyokusudiwa kwani ni kinyume cha sheria na watakaofanya hivyo watashitakiwa mahakamani.

Tayari kikosi kazi hicho kimefanikiwa kukamata betri 48 na watuhumiwa wawili wamekamatwa majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi.

story credit : Mroki Mroki

 


Comments




Leave a Reply