Shule ya Bloomington High huko nchini Marekani imeongeza rasmi lugha ya Kiswahili katika lugha kuu tano za kigeni. Suala hili limenifanya nijiulize sababu hasa ya kufanya hivi na hatimaye nimejiaminisha kuwa, lengo la kufanya hivi huenda ni kutaka vijana na watu wa Taifa la Marekani kuelewa lugha mbalimbali za dunia kadiri wanavyoweza ili waweze kuwasiliana na watu wa mataifa mbalimbali kwa urahisi zaidi. Pengine laweza kuwepo lengo lililojificha la kuwataka raia wake wajifunze lugha mbalimbali, lakini ukweli haupingiki ya kuwa haiwezekani kumzuia mtu kujifunza lugha nyingine ikiwa amekusudia, nasi cha msingi tunachoweza kukifanya ni kujifunza lugha zao ili kuweza kuwasiliana na watu wengi zaidi katika shughuli mbalimbali. Faida za kujifunza lugha za kigeni ni nyingi. Baadhi ya faida hizo ni pamoja na:
The main goal of the STARTALK Swahili student program is to introduce Swahili to Bloomington High schools, initially, as a nonresidential program. In the future we would like to offer it as a residential program and make it available to all Indiana high schools. The program will integrate the 5Cs of the National Foreign language Standards with a focus on the C of Communication and the C of Cultures. This will be a four week program with each week focusing on a particular cultural theme such as greetings, extended family, traditional clothes, food, and story telling. The first week will focus on greetings, introductions and talking about family members. The second week, students will learn about different kinds of food, ingredients required, and how to shop and bargain for them at the market. Week three will introduce students to the art of story telling using children’s stories and folktales. The last week of the four week program will concentrate on clothing with a focus on different uses of the traditional cloth, the kanga, and its sayings for indirect communication. This intensive program will be the equivalent of one semester of Swahili and students will get foreign language credits. 812-855-3323 • aomar@indiana.edu • www.indiana.edu/~afrilang CommentsSyanaloli 08/04/2010 9:56pm
Je ungewashauri nini watanzania wanaoibeza lugha yao hiyo inayoshika kasi katika nchi nyingi za Kiafrika na ulaya na sasahapa marekani.Wewe umeona hapo Indiana.Minnesota University pana kitivo cha Lugha ya kiswahili(Credit kabisa) na hata vyuo vikuu vingine hapa Marekani vinafundisha Kiswahili.Mimimwenyewe miaka ya 2001-2002 nilifundisha Kiswahili katika baadhi ya high school kule Ujerumani Munich.Hapa marekani community ya Waamerica weusi wamechagua lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya ya pili baada ya Kiingereza na wapo wanajifunza kwa bidii sana.
Reply
09/04/2010 8:30am
Hii ni changamoto kwetu sisi ambao Kiswahili ni lugha yetu mama.Sisi tulilazimishwa kujifunza kiingereza na kwa kuhofia sayansi na technologia pamoja na ajira za ndani na nje ya nchi tukakipa kiingereza msisitizo mkubwa na kukibeza kiswahili.
Reply
04/06/2010 8:12am
Natumai nyote hamjambo. Nikefuarahi kusoma maoni yenu. Program hii itawawezesha wanafunzi wa shule za sekondari za Bloomington, Indiana kujifunza lugha yetu na kuelewa tamaduni za watu wa Afrika ya Mashariki. Mimi ni mkurugenzi wa programu hii. Nitafundisha pia pamoja na walimu wengine wawili - Abdulwahid Mazrui na Meg Arenberg.
Reply
04/06/2010 8:22am
aaah, mwalimu Alwiya, salam sana na shukrani kwa kuthibitisha kuhusu hili, hasa kwa kuwa wewe ni mdau katika shule hiyo.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed