![]() Zoezi la sensa ya kuhesabu idadi ya watu wanaoishi nchini Marekani limeweka historia kwa kuitambua na kuiongeza lugha ya Kiswahili katika orodha ya moja ya lugha za Kimataifa zilizopewa kipaumbele na kuchapishwa rasmi kama mwongozo wa dodoso ili kufanikisha zoezi hili. Katika video iliyopo kwenye tovuti hiyo ambayo inatoa maelekezo kuhusu dodoso la sensa hiyo, mzungumzaji amekosea kidogo mahala fulani anaposikika akisema, '...masaba' badala ya 'saba' na mahala pengine ametamka, '...masita' badala ya 'sita' lakini kwa ujumla amesoma vizuri na katika lafudhi mojawapo ya Kibantu na inaeleweka. Bofya picha hapo kushoto (au bofya hapa) kutizama video hii. Ikiwa unataka nakala ya mwongozo huo wa sensa, unaweza kuipakua katika tovuti hiyo kwa lugha ya Kiswahili 2010.census.gov/2010census/language/swahili CommentsMonica 07/04/2010 1:12am
Congrants Swahili, it was first in East Africa only, now is taking chance!It should be included in University Curriculum to easen its spread!in every success there must be frontiers,Congrants to them!
Reply
11/06/2010 8:11am
Hii ni faraja kubwa sana kwa wadau na watetezi wa lugha ya Kiswahili.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed