
Zimetolewa tovuti mbadala ili kupambana na tatizo la traffic, hivyo jaribu katika mojawapo ya hizi zifuatazo:
Linki Na. 1 www.necta.go.tz/matokeo_acsee/Alevel
Linki Na. 2 admin.udsm.ac.tz/results/Alevel
Linki Na. 3 matokeo.necta.go.tz/matokeo_acsee/Alevel
Ijapokuwa katika matokeo hayo, wavulana wanaongoza katika kumi bora Kitaifa, lakini wastani wajumla unaonyesha wasichana wamefanya vyema zaidi ya wavulana.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako alisema ufaulu umepungua kwa asilimia 0.78 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2009 ambapo waliofaulu ni sawa na asilimia 89.64.
Alisema watahiniwa wa shule waliofaulu ni 45,217, sawa na asilimia 93.76 ya waliofanya mtihani na watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 10,547 sawa na silimia 74.57.


RSS Feed