Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika bwana Steven Wassira (aliyesimama akishikilia kijitabu) akichambua Mswada Sheria ya Madini wa mwaka 2010 ambao kwa mujibu wa ratiba ya mkutano wa 19 wa Bunge unatarajiwa kuwasilishwa bungeni. “Nchi inapata nini na wananchi watapata nini?... Je haiwezekani kuwawezesha watu maskini, wawekezaji wa ndani?” Aliuliza Waziri Wassira ambaye alisema kwamba ni kuwawezesha wawekezaji wa ndani ni muhimu huku akitoa mfano wa Sweden ambayo alisema uchumi wake unaotegemea madini kwa kuwezesha wachimbaji wake wadogo wazawa.
Waziri Mkuu bwana Mizengo Pinda (aliyeketi kwenye kiti kilichotandikwa kitambaa cheupe) na Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa (kulia) wakisafiri katika behewa la daraja la tatu kutoka stesheni ya Mpwapwa hadi Godegode kwenye Reli Ya Kati wakati Waziri Mkuu alipokagua ukarabati wa reli hiyo tarehe 18 Aprili 2010. Mafuriko yaliharibu vibaya reli hiyo na ukarabati wake unaendelea huku ukitarajiwa kukamilika katikati ya mwezi Mei ili kuruhusu kuanza tena kwa safari za kawaida za treni ya njia hiyo.
Photo credits: Beda Msimbe - Lukwangule Ent.




RSS Feed