Mchezo huo ulikuwa wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana na ulifanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
kwenye mchezo uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Vijana wa Ngorongoro Heroers walipigana vikali kuhakikisha wanaondoka na ushindi mnono dhidi ya wamalawi hao waliokuwa wakicheza mpira wa kiwango cha juu japokuwa umaliziaji wao haukuwa mzuri mara kadhaa walipofika langoni mwa Ngorongoro Heroers.
Iliwachukua dakika tatu tu vijana wa Ngorogoro Heroers kupata goli lililofungwa na mshambuliaji Omega Seme ambapo timu hiyo iliendelea kuleta madhara katika lango la Malawi na mara nyingine Thomas Ulimwengu aliipatia goli la pili. Magoli hayo yalifungwa kabla ya kipindi cha kwanza kwisha.
Kipindi cha pili kilianza na kuendelea hadi dakika ya mwisho ambapo Malawi walipata goli la kufutia machozi katika dakika ya tisini kwa njia ya penati, mpira uliyopigwa Lastin Simkonda baada ya Heroes kufanya 'madhambi' katika eneo la Malawi.
Goli hilo lilipandisha mori wa Ngorongoro Heroers ambapo ilicheza vizuri katika dakika za lala salama kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 91 pale Rashid Issa Rashid alipoukokota mpira mpaka wingi ya kushoto na kutoa pasi nzuri kwa Thomas Ulimwengu aliyeunganisha mpira huo na kuandika goli la tatu.
Hivyo hadi mwisho wa mchezo ni Ngorongoro Heroes 3 na Malawi 1.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa nchini Malawi, timu hizo zilitoka sare ya kufungana magoli mawili kila moja.
Kwa matokeo hayo basi, timu ya ngorongoro itakutana na timu ya vijana ya Ivory Coast wiki ya tatu ya mwezi mei ambapo mchezo wa kwanza utafanyika katika nchini Ivory Coast na baada ya wiki mbili timu hizo zitarudiana katika dimba uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Habari kwa mujibu wa John Bukuku na Picha kwa hisani ya Issa Michuzi.










RSS Feed