RUKSA POMBE YA 'mnazi' Kenya 12/04/2010
![]() William Ruto (W) - Kilimo Kenya Haiya sasa, habari ndiyo hii. Waziri wa Kilimo wa Kenya bwana William Ruto ametoa ruhusa kutumia pombe ya Pwani al maaruf 'mnazi', kwa kuwa ni mojawapo ya utamaduni wa Waswahili wa Pwani. Habari kwa mujibu wa TBC1, bofya kifute hapo usikilize. YATOKANAYO Nakumbuka mchangiaji mmoja wa habari katika kundi pepe fulani hivi majuzi, nadhani wiki mbili tu zilizopita, aliandika na kuhoji kwa kirefu tu sababu za ni kwa nini angekuwa kiongozi angeruhusu utengenezaji halali na matumizi ya pombe aina ya 'gongo' iliyozoeleka nchini Tanzania. Pamoja na mengi, alisema pombe hii itakuwa chanzo cha ajira kwa wanaoitengeneza, itakuwa zao la biashara kama zilivyo Konyagi, Valeur na aina nyingine ya 'gin' vile vile alisisitiza kuwa kuhalalisha pombe hii kutaondoa utengenezaji haramu ambao ni hatari. Nadhani mawazo yake yalipitishwa kutoka akilini Tanzania hadi kwenye matendo Kenya. Hii nayo imenikumbusha tena kauli aliyoiandika bwana mmoja katika mdahalo ule, '...sisi Watanzania ni wazuri sana wa kutengeneza sera, Rwanda ni wazuri wa kutekeleza sera zetu'. Hii nchi hii, mi sijui tena bana. | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed