Maisha ya binadamu ya kuhama haka toka eneo moja hadi jingine ni ya tangu karne na vizazi hata vizazi. Angalabu watu wamekuwa wakihama ili kukidhi haja za kimaisha hasa pale walipo panapokosekana namna ya kutimiza mahitaji hayo ama kunapokuwa na usumbufu mkubwa, kama vile siasa chafu, uongozi mbovu, hali ya hewa isiyostahimilika, machafuko katika jamii, nk, yanayosababisha ugumu katika kukimu uhitaji na kufikia malengo mengineyo. Mipaka ya kijiografia, sheria za nchi na makubaliano baina ya mataifa juu ya rushusa na pasi na vibali vya kusafiria kuvuka mpaka mmoja kwenda kwingien imekuwa vimekuwa vizuizi vya safari nyingi ambazo zingeweza kufanyika kiholela. Najaribu kuifikiria dunia isiyo na vizuizi, taswira bado hainijii...

Nimewaza hivi kufuatia kuziona picha zilizopigwa na mwandishi Francis Godwin na kubandikwa kwenye blogu yake zikionesha baadhi ya raia wanaosadikiwa kuwa wanatoka nchini Ethiopia na Somalia, punde walipokamatwa katika msako na askari polisi kwa kosa la kuwepo nchini Tanzania bila vibali maalum.
 


Comments




Leave a Reply