Wale wote mnaofuatilia mitandao jamii ya video mtagundua kuwa TED ni mojawapo ya mitandao bora kabisa elimishi katika jamii. Ni sehemu ambayo utapata kujifunza mengi ambayo hayajawahi kuzungumzwa jukwaani mahali pengine (ndiyo mojawapo ya misingi ya TED) katika maisha ya kila siku, tangu kuelezea mambo ya kihistoria hadi uvumbuzi mpya wa kisayansi, upigaji picha hadi utunzi wa mashairi. Katika tovuti hii tumekuwa tukiweka baadhi ya video zinazovutia na kuendana na mazingira yetu (
unaweza kuziona katika ukurasa wa videos) na mojawapo maarufu sana ni zile za mwalimu
Hans Rosling anavyopambanua takwimu mbalimbali za kimaendelo katika maisha ya binadamu katika mataifa ya dunia kwa miaka kadhaa.
Habari njema ni kuwa, kwa mara nyingine tena TED watakuwepo Tanzania, ila safari hii si sawa na wakati walipokuja kama TED ambapo ilikuwa ni mkutano mkubwa, bali wanakuja kama TEDx kwa mfumo mpya wa kujigawa na kutembelea maeneo mengi zaidi.
In the spirit of ideas worth spreading, TED has created a program called TEDx. TEDx is a program of local, self-organized events that bring people together to share a TED-like experience. Our event is called TEDx Dar "Pamoja Tunaweza!", where x=independently organized TED event. At our TEDxDar event, TEDTalks video and live speakers will combine to spark deep discussion and connection in a small group. The TED Conference provides general guidance for the TEDx program, but individual TEDx events, including ours, are self-organized. Soma zaidi kuhusu TEDxDar event kupitia:
www.tedxdar.com